Wizi mafuta reli ya kisasa washika kasi, polisi waingilia kati

February 6, 2023 11:18 am · Mariam John
Share
Tweet
Copy Link
  • Polisi yakamata mafuta aina ya dizeli lita 850.
  • Yameibwa katika nyakati tofauti wakati ujenzi wa reli ya kisasa ukiendelea.

Mwanza. Jeshi la Polisi mkoani Mwanza, linawashikilia watu wanne kwa tuhuma za kuiba vifaa mbalimbali vya mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) yakiwamo mafuta ya dizeli lita 850.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Wilbroad Mutafungwa amesema watuhumiwa hao walikamatwa katika oparesheni iliyoanza Januari 11 hadi Februari 3, 2023 walipofanikiwa kuwakamata watu hao.

Amesema katika oparesheni hiyo walimkamata Wilbert Constantine (30) mkazi wa kijiji cha Mantare wilayani Magu akiwa na madumu 55 yenye ujazo wa lita 20 kila moja yakiwa yamefichwa kwenye kibanda nyumbani kwake.

“Katika kibanda hicho pia yalikutwa mapipa matatu matupu, mipira ya kunyonyea mafuta na keni za kupimia mafuta,” amesema Mutafungwa.

Kamanda Mutafungwa amesema katika kijiji cha Mantale wilayani Kwimba polisi walifanya msako na kukamata madumu 16 yenye mafuta aina ya dizeli lita 320 yaliyokuwa yamefichwa shambani.

Aliongeza kuwa polisi wanamshikilia Pascal Abdallah (20)  mkazi wa Salawi mkoani Shinyanga kwa tuhuma za kubeba mafuta ya dizeli lita 190 kwenye pikipiki, huku mwingine akikimbia na kutelekeza madumu ya mafuta lita 200.

Mkazi mwingine Mihambo Elias alikamatwa baada ya kukutwa na madumu matupu  10 dukani kwake kwenye nyumba ya Warwa Charles.


Soma zaidi: 


Katika msako huo pia polisi walimkamata Stephano Jacob (35), mkazi wa Salawi  mkoani Shinyanga  kwa kutajwa kwamba ndiye mwenye mzigo aliokamatwa nao Pascal Abdallah.

Kamanda Mutafungwa amesema oparesheni hiyo bado inaendelea katika maeneo yote yanayozunguka mradi wa SGR.

Aliwaomba wananchi katika maeneo hayo ya mradi kutoa taarifa kuhusu wahalifu wanaoiba vifaa mbalimbali vya SGR ili wakamatwe na kukomesha wizi unaofanywa na watu hao.

Lengo la reli hiyo inayotoka Dar es Salaam hadi Mwanza kisha Kigoma ni kuongeza ufanisi katika sekta ya usafirishaji nchini ususani sekta ya reli ambapo itabeba mzigo wa mpaka tani 10,000 kwa mkupuo sawa na uwezo wa maroli 500 ya mizigo na kuokoa muda wa usafirishaji abiria na mizigo.

Pia itachangia katika ongezeko la ajira kwa wazawa katika sekta na fani mbalimbali na uboreshaji wa huduma za kijamii ikihusisha ujenzi wa shule, vituo vya afya na ujenzi wa barabara katika maeneo yanayopitiwa na mradi huo.

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Wabunge waliokwenda Morocco bila kibali kikaangoni , utoro ukiibuliwa bungeni

Wabunge waliokwenda Morocco bila kibali kikaangoni , utoro ukiibuliwa bungeni

Nukta TV

Mfahamu Leonard Mususa Alama ya Ungozi iliyoacha majonzi kwa 'MACEOs' Tanzania

Mfahamu Leonard Mususa Alama ya Ungozi iliyoacha majonzi kwa 'MACEOs' Tanzania

Nukta TV

Bei za mafuta mwezi Juni hizi hapa, dizeli ikipaa kwa Sh85

Bei za mafuta mwezi Juni hizi hapa, dizeli ikipaa kwa Sh85

Nukta TV