WCF yakutana na madaktari kufanya tathmini ya ulemavu kazini

May 23, 2023 1:00 pm · Mariam John
Share
Tweet
Copy Link
  • Wakutana jijini Mwanza kujadili namna ya kuwasaidia wafanyakazi wanaopata ajali, magonjwa kazini.

Mwanza. Jumla ya madaktari 100 kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa wameshiriki mafunzo ya tathmini ya ulemavu unaotokana na ajali na magonjwa yatokanayo na kazi lengo ikiwa ni kuwajengea uwezo ili waweze kuwasaidia watu waliopata majanga kwenye maeneo ya kazi.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tano ya kuwajengea uwezo madakatari hao leo Mei 23, 2023, Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Hassan Masala amesema lengo ni kuhakikisha tathmini hizo zinafanyika kwa usahihi na wale wafanyakazi walioumia au kuugua wanapata stahiki zao kwa wakati.

Masala amesema kimsingi Serikali ilianzisha Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) kwa lengo la kuhakikisha wafanyakazi wanapata mafao bora ya fidia tofauti na ilivyokuwa sheria ya zamani ya fidia kwa wafanyakazi.

Kwa mjibu wa sheria ya zamani kiwango cha juu cha fidia alichokuwa anapata mfanyakazi aliyepata ajali ilikuwa Sh108,000 au Sh83,000 kwa mfanyakazi aliyefariki na ajali au ugonjwa kazini.

“Kiwango hiki kimepitwa na wakati sana hivyo kuifanya sheria ya zamani kutokidhi mahitaji ya sasa,” amesema Masala na kuongeza

“Mfuko huo kwa sasa una faida kubwa kwa wafanyakazi ambapo hivi sasa wana uhakika wa kinga ya kipato kutokana na majanga yanayosababishwa na ajali, magonjwa au kifo yanayotokana na kazi huku waajiri wanapata muda wa kushughulikia masuala ya uzalishaji na uendelevu wa biashara zao pindi mfanyakazi anapougua au kufariki kutokana na kazi.”

Faida nyingine ya mfuko huo ni kuongezeka kwa pato la Taifa inayotokana na kukua kwa tija na uzalishaji mahala pa kazi.

Hata hivyo, mkuu huyo wa wilaya ametoa wito kwa mfuko huo kuendelea kutoa elimu ya masuala ya fidia ya wafanyakazi ikiwa ni  pamoja na mafunzo kwa madaktari ambao ni kiungo muhimu pamoja na wahanga wa ajali na wagonjwa wanaotokana na kazi zao.

“Awali, mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Abdulsalaam Omar amesema mafunzo haya yameandaliwa kama sehemu kuuwezesha mfuko kutekeleza vyema jukumu la kufanya tathimini sahihi na kwa wakati pindi mfanyakazi anapoumia au kuugua kutokana na kazi.

“Uelimishaji wa aina hii ni moja ya mikakati ya kuondoa changamoto ambazo zinaukabili mfuko huo,” amesema Omar.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
25 Sep, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
26 Sep, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
26 Sep, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Lissu alivyotumia saa tisa kujitete mahakamani, aibua hoja tatu nzito

Lissu alivyotumia saa tisa kujitete mahakamani, aibua hoja tatu nzito

Nukta TV

Walimbwende ‘Miss World’, kupewa makabila Tanzania kuwakilisha kimataifa

Walimbwende ‘Miss World’, kupewa makabila Tanzania kuwakilisha kimataifa

Nukta TV

Makonda: Jezi ya Taifa Stars mbaya, hangaikeni  iwe nzuri

Makonda: Jezi ya Taifa Stars mbaya, hangaikeni iwe nzuri

Nukta TV