Waziri Mkuu wa Uingereza ajiuzulu baada ya kukaa ofisini kwa siku 45

October 20, 2022 1:01 pm · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Amesema asingeweza kutimiza ahadi alizotoa alipokuwa akiwania nafasi ya kuwa kiongozi mkuu wa chama cha Conservative ili kumuwezesha kuwa waziri mkuu.

Dar es Salaam. Liz Truss, Waziri wa Uingereza amejiuzulu muda mfupi uliopita na kuweka historia ya waziri mkuu aliyekaa madarakani muda mfupi nchini humo.

Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), Waziri Mkuu wa  pili aliyehudumu kwa muda mfupi zaidi alikuwa George Canning, alihudumu kwa siku 119 baada ya kufariki dunia.

Trus katika hotuba yake ya kujiuzulu leo Oktoba 20, 2022 mbele ya ofisi yake amesema asingeweza kutimiza ahadi alizotoa alipokuwa akiwania nafasi ya kuwa kiongozi mkuu wa chama cha Conservative ili kumuwezesha kuwa waziri mkuu.

“Tuliweka maono ya kodi ya chini na wa ukuaji wa juu wa uchumi ambao utachukua fursa ya uhuru wa Brexit.”

“Lakini ninatambua, kutokana na hali hiyo, siwezi kutoa mamlaka ambayo nilichaguliwa na Chama cha Conservative. Kwa hiyo nimezungumza na Mtukufu Mfalme kutangaza kwamba ninajiuzulu kama kiongozi wa Chama cha Conservative,” amesema.

Duru za kimataifa zinaeleza kuwa kujiuzulu kwake kumetokana kufeli kwa mpango wake wa kiuchumi uliosababisha mtikisiko wa masoko ya kifedha na kukigawa chama chake.

Kujiuzulu kwake kumetanguliwa na mfululizo wa matukio ya fujo ndani ya chama chake ambapo baadhi ya wanachama wamekuwa wakimshinikiza ajiuzulu, licha ya yeye kutotaka kufanya hivyo.

Jana jioni Oktoba 19, 2022 Waziri wa Mambo ya Ndani Suella Braverman, alijiuzulu akiwa ni waziri wa pili kuondoka katika baraza la mawaziri la Waziri Mkuu Liz Truss.

Mapama leo asubuhi, waziri mwingine aliwasilisha barua ya kutokuwa na imani na Trus.

Waziri Mkuu mpya anatarajiwa kuteuliwa wiki ijayo. Hata hivyo, kiongozi wa upinzani Keir Starmer ametaka uchaguzi mkuu ufanywe.

Truss alichukua wadhifa huo baada ya Boris Johnson ambaye pia alilazimika kujiuzulu kutokana na kashfa mbalimbali ikiwemo kukiuka kanuni za kujikinga na Uviko-19.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jul, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Kutana na ‘Poultry Plucker’, mashine inayonyonyoa kuku watatu kwa dakika moja

Kutana na ‘Poultry Plucker’, mashine inayonyonyoa kuku watatu kwa dakika moja

Nukta TV

Rais Samia: Kalamu yangu ina hatari, sijawahi kusaini mtu kunyongwa

Rais Samia: Kalamu yangu ina hatari, sijawahi kusaini mtu kunyongwa

Nukta TV

Rais Samia: Matumizi jina Samia, likiwa kila mahali inachosha, tafuteni wengine

Rais Samia: Matumizi jina Samia, likiwa kila mahali inachosha, tafuteni wengine

Nukta TV