Waziri Jafo awataka watafiti kutoa elimu mbegu za kibayoteki

October 26, 2022 6:49 am · Daniel Samson
Share
Tweet
Copy Link

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dk Selemani Jafo akizungumza Oktoba 25, 2022 jijini Dar es Salaam katika ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa mwaka na Uzinduzi wa Chama cha Bioteknolojia Tanzania (BST). Picha | Daudi Mbapani.


  • Asema bado kuna hofu na mkanganyiko kuhusu mbegu hizo.
  • Asema hakuna haja ya kuzuia tafiti bali watu wapanue mjadala.

Dar es Salaam. Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dk Selemani Jafo amewataka watafiti na wasomi kuja na majibu ya uhakika yatakayosaidia kuondoa hofu kwa baadhi ya Watanzania juu matumizi ya mbegu za kibayoteki zinazotokana na teknolojia ya uhandisi jeni (GMO).

Mazao ambayo yanazalishwa kwa wingi kupitia teknolojia ya GMO ni pamoja na mahindi, pamba, maharage ya soya na viazi ambavyo hutegemewa na nchi za Afrika kama sehemu ya kuboresha usalama wa chakula na kuingiza kipato.

Hata hivyo, kumekuwa na uelewa na dhana tofauti kuhusu matumizi ya mbegu hizo kwenye shughuli za kilimo huku wanaopendekeza wakisema wakulima wakitumia zitawasaidia kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya hali ya hewa ambayo yameathiri shughuli za kilimo katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo kupungua kwa mvua. 

Pia zinazaliana sana kuliko mbegu za asili na zinaweza kuongeza uzalishaji na soko kwa wakulima.

Baadhi ya wataalamu wa mazingira na afya ya binadamu wamezikataa mbegu hizo na kudai kuwa zinaathiri afya ya binadamu, ukuaji wa akili ya watoto na ni chanzo kikubwa cha uharibifu wa mazingira.

Kutokana na maoni tofauti kuhusu GMO, Waziri Jafo amewashauri wasomi na watafiti kupanua wigo wa mjadala wa suala hilo na kutoa majibu ya uhakika ili kuondoa hofu zilizopo kwenye jamii kama ilivyofanyika kwa janga la Uviko-19. 

Amesema hofu hizo huenda zinasababishwa na vitu vingi ikiwemo maslahi ya kibiashara ambapo baadhi ya watu wanahofia shughuli zao zinaweza kufa ikiwa mbegu hizo zitatumika kwenye shughuli za kilimo. 

Jafo aliyekuwa akizungumza leo Oktoba 25, 2022 jijini Dar es Salaam katika ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa mwaka na Uzinduzi wa Chama cha Bioteknolojia Tanzania (BST) amesema wakati mwingine hofu inakuja kwa sababu wananchi hawana elimu ya kutosha kuhusu mbegu hizo.

“Watu wapate elimu iliyokuwa pana zaidi ya kuondoa mashaka, ni kazi ya watafiti kulifanya suala hilo. Hili suala lina mambo nengi kwanza hofu, la pili ni jambo la kibiashara, watafiti mfungue mlango watu waelewe kwa kina jinsi gani tunakwenda mbele,” amesema Dk Jafo.


Soma zaidi:


Amesema mapendekezo ya wasomi na watafiti hao yatakapoletwa mezani, ndiyo yataamua nchi iendelee mbele au iachane na GMO lakini tafiti na mijadala kuhusu suala hilo havipaswi kuzuiwa kwa sababu binadamu anatakiwa kujifunza kila wakati ili kufanya maamuzi sahihi.

Aidha, amesema wizara yake iko tayari kutoa ushirikiano ikiwemo kufanya mabadiliko ya kanuni kuhakikisha tafiti za kisayansi GMO zinafanyika kwa weledi bila kuathiri mazingira na uchumi wa nchi.

“Ofisi yetu iko tayari kuhakikisha inashirikiana na wadau wote kwa maslahi mapana ya nchi yetu ya Tanzania,” amesema Jafo. 

Kulingana na sheria ya Usimamizi wa Mazingira ya mwaka 2004 kifungu cha 69 (1) – (3) kimeweka kanuni ambazo zinazozuia uingizaji wa vifaa vya kutengeneza mbegu hizo kwa ajili ya utafiti ambapo mtu yeyote atakayeingiza mbegu za GMO atawajibika kwa madhara yatakayotokea kwa afya za watu na mazingira. 

“Chama chetu kimebaini kuwa uelewa na ufahamu wa baadhi ya wadau kuhusu matumizi ya bidhaa zitokanazo na biteknolojia ni mdogo na hii imesababisha ongezeko la taarifa zisizo sahihi kuhusu teknolojia hii zenye kuleta hofu kwa jamii ya Watanzania ,” amesema Mwenyekiti wa BST, Profesa Peter Msolla.

Amesema BST itaendelea kutoa elimu kwa kuwaleta pamoja wadau mbalimbali ili kuwa na uelewa wa pamoja kuhusu GMO na namna inavyoweza kuifadisha Tanzania. 

Baadhi ya washiriki na wanachama wa Chama Cha Bioteknolojia Tanzania (BST) waliohudhuria ufunguzi wa mkutano mkuu wa chama hicho jana Oktoba 25, 2022 jijini Dar es Salaam. 

Amesema changamoto za mabadiliko ya tabianchi siyo nadharia tena kwa sababu zimeenea dunia, hivyo ni muhimu kuja na teknolojia itakayosaidia sekta ya kilimo kustawi na kukua ili kuwafaidisha wakulima.

Majaribio ya mbegu za GMO yaliingia Tanzania mwaka 2008 chini ya mradi wa Water efficient Maize for Africa (WEMA) uliofadhiliwa na taasisi ya Bill&Merinda Gates ya nchini Marekani lakini yalianza kufanyika mwaka 2016 katika Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Makutupora (TARI) lakini Serikali ilisitisha kwa muda na bado haijaridhia matumizi ya mbegu hizo kwa wakulima.

Kwa mujibu wa Huduma ya Kimataifa ya Upataji wa Maombi ya Kilimo kibayoteki (ISAAA), hadi kufikia mwaka 2020, nchi 31 duniani zilikuwa zinalima mazao ya kibayoteki, huku nchi mbalimbali zikiendelea na utafiti wa mbegu hizo kabla hazijapelekwa kwa wakulima. 

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
13 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
13 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
13 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: HII HAPA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027

🔴LIVE: HII HAPA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027

Nukta TV

Mashine za kukaushia rangi za kucha kutozwa ushuru kwa asilimia 10

Mashine za kukaushia rangi za kucha kutozwa ushuru kwa asilimia 10

Nukta TV

Wazee wa 'kubet' hii inawahusu, 5% kutozwa kwenye dau la kamari

Wazee wa 'kubet' hii inawahusu, 5% kutozwa kwenye dau la kamari

Nukta TV