Watu wanaoishi karibu na mbuga za wanyama wana afya bora: Ripoti

May 30, 2019 7:25 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link

Kuwa na afya njema ni zaidi ya kula vizuri na kufanya mazoezi bali ni pamoja na kuishi katika eneo zuri lenye mazingira ya asili. Picha|Mtandao.


  • Utafiti uliofanywa na Chuo Cha Taifa cha Oregon nchini Marekani unaeleza kuwa maeneo hayo yaliyohifadhiwa yana utajiri wa asili kwa ajili ya afya ya binadamu.
  • Ni maeneo yenye utulivu na mandhari nzuri kuliko maeneo mengine. 
  • Afya bora ni zaidi ya kula chakula na kufanya mazoezi bali mazingira mazuri ya kuishi.

Yamezungumzwa mengi kuhusu umuhimu wa kula chakula bora chenye virutubisho  na kufanya mazoezi ili kuwa na afya njema na ustawi mzuri wa maisha.

Lakini ni nadra kusikia kuwa kuishi karibu na maeneo yaliyotengwa maalum na kuhifadhiwa kama mbuga za wanyama, misitu ya asili ni njia nyingine inayotumika kuboresha afya za watu. 

Watafiti wa Chuo cha Taifa cha Oregon cha nchini Marekani, wamebaini kuwa kuishi karibu na ardhi iliyohifadhiwa ambayo inajumuisha hifadhi za Taifa, mapori ya akiba, na mbuga za wanyama kuna matokeo chanya kwa afya ya binadamu. 

Watafiti hao wanaeleza kuwa watu wanaoishi kwenye maeneo yaliyohifadhiwa wananufaika na uhifadhi wa muda mrefu na faida hiyo huongezeka wakati eneo lilohifadhiwa linapokuwa na matumizi mengi, kwa sababu wakazi wanaweza kupata na kutumia fursa za asili za eneo husika.. 

Mtaalam wa mazingira katika Chuo hicho, Drew Gerkey  amesema mipaka ya maeneo ya uhifadhi iko katika hali inayoruhusu watu wanaoishi karibu kupata mandhari nzuri ambayo inahitajika kwa binadamu japo hawawezi kuishi ndani ya maeneo hayo. 

Gerkey amesema maeneo yaliyohifadhiwa yenye vivutio vya utalii kama hifadhi za Taifa yana zaidi ya utajiri wa asili kwa asilimia 17 ukilinganisha na kaya ambazo ziko mbali na maeneo hayo.


Zinazohusiana: 


Matokeo ya utafiti huo ni muendelezo wa mazungumzo juu ya athari za uharibufu wa maeneo yaliyohifadhiwa ambayo ni muhimu kwa maisha ya viumbe hai. 

Kwa mujibu wa taasisi ya Ontario Nature ya nchini Canada, maeneo yaliyohifadhiwa yana faida nyingi ikiwemo kutoa hali ya hewa nzuri, dawa za asili, burudani na utulivu ambao ni muhimu kwa maendeleo ya mwanadamu. 

Kuwa na afya njema ni zaidi ya kula vizuri na kufanya mazoezi bali ni pamoja na kuishi katika eneo zuri lenye mazingira ya asili. 

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
5 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
5 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

Nukta TV

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Nukta TV

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

Nukta TV