Watanzania waishio nje ‘watasubiri sana’ kushiriki uchaguzi wa ndani

May 23, 2019 1:29 pm · Daniel Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Serikali imesema bado inaandaa sera na ikikamilika italijulisha Bunge na wananchi wote. 
  • Imesema inatathmini idadi ya Watanzania waliopo nje na shughuli wanazofanya.
  • Huenda Watanzania hao wasipate fursa ya kushiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu.

Dar es Salaam. Watanzania wanaoishi nchi za nje wataendelea kusubiri kwa muda usiojulikana kupata fursa ya kushiriki chaguzi za ndani wakiwa nje baada ya Serikali kusema kuwa bado inaandaa sera na kutathmini ili kuona kama utaratibu huo unafaa.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo (Mei 23, 2019) wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti maalumu (CCM), Asha Juma aliyetaka kujua ni lini Serikali itakamilisha utaratibu wa kuwawezesha Watanzania wanaoishi nchi za nje kuweza kupata nafasi yao ya kidemokrasia ya kupiga kura.  

“Jambo hili ni la kisera na Serikali imeendelea kuona kama utaratibu huo unaweza kufaa kwa sababu lazima tupate kujua nani wako nje ya nchi, idadi yao, wanafanya shughuli gani, na je kama bado ni Watanzania au waliomba urai wa kule nchi za nje,” amesema Majaliwa. 


Soma zaidi: 


Majaliwa amesema pindi sera hiyo itakapokamilika pale itakapoonekana inafaa, Serikali itawajulisha Watanzania na Bunge.  

Hata hivyo, Waziri Mkuu hajawaweka wazi ni lini sera hiyo itakamilika, jambo ambalo linawaweka katika wakati mgumu Watanzania hao waishio nje kama wanaweza kushiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika mwaka huu na Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani utakaofanyika mwaka 2020.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
26 Jul, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
27 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
27 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Hizi ndio passport 5 zenye nguvu zaidi duniani

Hizi ndio passport 5 zenye nguvu zaidi duniani

Nukta TV

Hii ndio spirulina: Hazina ya maji inayoboresha afya za Watanzania

Hii ndio spirulina: Hazina ya maji inayoboresha afya za Watanzania

Nukta TV

Mradi wa Sh4.6 bilioni kutoa ahueni ya umeme Lindi, Mtwara

Mradi wa Sh4.6 bilioni kutoa ahueni ya umeme Lindi, Mtwara

Nukta TV