Wafanyabiasha kuneemeka na ‘flyover’ ya Gerezani

January 23, 2019 4:29 pm · Daniel
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni wale wanaofanya biashara katika eneo la Kariakoo na maeneo ya jirani kwasababu itawapunguzia adha ya foleni na usafirishaji wa mizigo.
  • Daraja hilo litajengwa kwa miezi 24 na kugharimu Sh25.28 bilioni chini ya mkandarasi kutoka Japan.

Dar es salaam. Huenda wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wanaofanya biashara katika eneo la Kariakoo na maeneo ya jirani wakapata ahueni ya foleni, baada ya Serikali kuanza mchakato wa ujenzi wa daraja la juu la Gerezani.

Hatua hiyo inakuja ikiwa imepita miezi mitano tangu kuzinduliwa kwa daraja la juu la  Mfugale (Mfugale flyover) ambalo limesaidia kupunguza adha ya foleni katika makutano ya barabara ya Mandela na Nyerere huku ujenzi wa daraja lingine la Ubungo ukiendelea.  

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (Tanroads) Mhandisi Patrick Mfugale amesema mradi huo unatarajiwa kujengwa kwa miezi 24 ambapo utagharimu Sh25.28 hadi kukamilika kwake.

Mhandisi Mfugale amebainisha kuwa ujenzi wa mradi huo ni sehemu mkakati wa kupunguza foleni barabarani na kampuni ya Sumitomo Mitsui Construction (SMCC) kutoka Japan ndiyo imepewa jukumu la ujenzi huo.

Daraja hilo litakalokuwa na urefu wa mita 40 na upana wa mita 30.4 na uwezo wa kuunganisha barabara za njia sita litasaidia kupunguza foleni hasa katika barabara za Uhuru, Msimbazi na Gerezani ambazo zimekuwa na msongamano nyakati za asubuhi na jioni.

Hali hiyo itaharakisha usafirishaji wa abiria na mizigo katika soko la Kariakoo ambalo linategemewa na wakazi wengi wa Jiji hilo kujipatia huduma na bidhaa mbalimbali ili kukidhi mahitaji ya kibiashara na familia.

Kampuni hiyo ya SMCC ndiyo iliyojenga daraja la juu la Mfugale lenye urefu wa mita 425 na uwezo wa kufanya kazi kwa takribani miaka 100 ijayo na kugharimu Sh106 bilioni. 

HALI YA FOLENI KATIKA ENEO LA GEREZANI NA TAZARA JIJINI DAR ES SALAAM

Kukamilika kwa daraja hilo huenda kukazaa matunda kama ilivyo kwa daraja la juu la Mfugale ambalo kwa mujibu wa data za kampuni ya Google za Januari mwaka huu zinaonyesha kuwa tangu kujengwa kwa daraja hilo foleni katika makutano ya barabara za Mandela na Tazara imepungua.

Lakini inaweza kuwa maumivu kwa wafanyabiashara wadogo na machinga ambao wamekuwa kipanga bidhaa zao pembezoni mwa eneo la Gerezani kwasababu watalazimika kuondoka na kupisha ujenzi huo. 

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
19 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
19 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Siku ya Familia, Mtoto wa Afrika kuadhimishwa Juni 30, 2026

Siku ya Familia, Mtoto wa Afrika kuadhimishwa Juni 30, 2026

Nukta TV

Wadau wa 'kubet" watoa ya moyoni, pendekezo kupanda kwa tozo 5%

Wadau wa 'kubet" watoa ya moyoni, pendekezo kupanda kwa tozo 5%

Nukta TV

Wasemayo wananchi, vocha za kukwangua kupigwa maruku mijini

Wasemayo wananchi, vocha za kukwangua kupigwa maruku mijini

Nukta TV