Wadau wa teknolojia watofautiana ujenzi mji wa ‘Silicon Dar’

January 8, 2019 11:23 am · Zahara
Share
Tweet
Copy Link

Eneo hili lililopo jijini Dar es Salaam ndiyo linatajwa kuwa kitovu cha shughuli za teknolojia kutokana na kusheheni kwa makampuni mbalimbali zikiwemo za simu na vituo atamzi.Picha| Fredy Njeje


  • Baadhi yao washauri mji huo ujengwe nje ya Jiji ili kuwakutanisha wabunifu sehemu moja kuendeleza vipaji vyao
  • Wengine wamesema itachukua muda kwa mji huo kukamilika kwasababu unahitaji uwekezaji mkubwa.
  • Serikali yashauriwa kuboresha sera na sheria ili kuwawezesha vijana kunafaika na rasilimali za teknolojia zilizopo nchini. 

Dar es Salaam. Suala la Jiji la  Dar es Salaam hasa maeneo ya kandokando ya barabara ya Old Bagamoyo na Ali Hassan Mwinyi kuitwa mji wa ‘Silicon Dar’  limeibua mawazo mchanganyiko kutoka kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii huku baadhi yao wakishauri kujengwa mji rasmi nje ya jiji hilo.  

 Eneo hilo limeanza kujipatia umaarufu kutokana na kuwepo kwa majengo marefu ya kifahari ambayo yanatumiwa na kampuni za teknolojia zikiwemo za mawasiliano ya simu kama Vodacom, Tigo, Halotel na Airtel. 

Pia kunapatikana vituo vingi vya kijamii na atamizi za kukuza ubunifu wa teknolojia, ujasiriamali ikiwemo Buni hub, Sahara Ventures,  Atamizi ya Biashara na Teknohama (DTBi), Smart Lab, SeedSpace wakiongozwa na Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH).

Kutokana na miundombinu iliyopo, baadhi ya wadau wa teknolojia wanasema kama eneo hilo litaendelezwa linaweza kufanana na mji wa ‘Silicon Valley’ uliopo katika Jiji la California nchini Marekani ambao umesheheni shughuli nyingi za teknolojia na ubunifu.

Lakini wengine wanafikiri siyo sahihi kulipa eneo hilo hadhi hiyo badala yake Serikali na wadau wa maendelea watafute eneo maalumu nje ya jiji hilo na kujenga mji ambao utatumika kama kituo kitakachowakutanisha wabunifu na wajasiriamali wa teknolojia kuendeleza vipaji na uvumbuzi wa njia mbalimbali za kutatua changamoto za jamii. 

 Wadau hao ambao wametoa maoni yao katika mtandao wa Twitter, wanaeleza kuwa ikiwa ndoto za kujenga mji huo zitafanikiwa ni vema ukapewa jina ambalo linasadifu ubunifu na maendeleo ya watanzania kuliko kuiga majina kutoka nchi zilizoendelea.

 “Silicon Dar ni jina baya kwa kweli, kwani teknolojia kwa Kiswahili ni nini? Jina linaweza kutengenezewa from there (kutokea hapa)” ameandika mchangiaji anayetambulika kwa jina la Ms. Saysa katika mtandao wa Twitter.


Zinazohusiana: 


Wanaeleza zaidi kuwa ikiwa wabunifu watajengewa mji huo na kukaa sehemu moja itarahisisha upatikanaji wa huduma kuliko hivi sasa ambapo vituo vya ubunifu vinajitegemea na viko maeneo tofauti. 

“Kama ningekuwa na mamlaka ningejenga mji wa teknolojia nje ya jiji yenye miundombinu inayohitajika,” ameandika Kennedy Mmari katika ukurasa wa Twitter.

Mmari anaongeza ili kuwaendeleza wabunifu hao, Serikali ifikirie kuwapa mapumziko ya kodi kwa muda, kuboresha sheria na kanuni mbalimbali wakati wa majaribio.

 Image result for silicon valley

 Mji wa ‘Silicon Valley’ uliopo katika Jiji la California nchini Marekani ambao umesheheni shughuli nyingi za teknolojia na ubunifu. Picha| tech gadget

Wakati wachangiaji hao wakihimiza mabadiliko hayo, wengine wamesema huenda ikachukua muda kwa mji huo kukamilika kutokana na gharama kubwa za kujenga miundombinu na utayari wa wabunifu wote kukubali kwenda katika mji huo ambao utakuwa umejitenga na huduma nyingine za taasisi za utawala na mashirika wa maendeleo. 

“Labda wameona kuweka nje ya jiji kuna changamoto nyingi, mfano kasi ya mtandao ukitoka nje ya mji ni ndogo sana hasa ile ya 4G,” ameandika Paul Lusambo, katika ukurasa wa Twitter.

Kenya tayari imeanza Kujenga mradi mkubwa wa mji wa teknolojia wa Konza Technology City nje kidogo ya jiji la Nairobi lakini itachukua muda kukamilika na kuanza kutoa huduma muhimu. 

Mkurugenzi Mtendaji wa Sahara Ventures, Jamanne Mtambalike ambaye amekuwa mstari wa mbele kupigania kujengwa kwa mji wa ‘Silicon Dar’ amesema ni wakati muafaka kwa ndoto hiyo kutimia kwasababu  jiji la Dar es Salaam linafikika kirahisi na itasaidia wabunifu kutoa huduma kwa watu wengi. 

Kupitia makala  iliyochapishwa katika mtandao medium, ameeleza kuwa wawekezaji wameonyesha nia ya kuuendeleza mradi huo mkubwa wa ‘Silicon Dar’ na ni vema wadau waungane kutimiza ndoto hiyo iliyokuwa inasubiriwa kwa muda mrefu.

Amebainisha kuwa jiji hilo tayari lina miundombinu rafiki kwa wabunifu na mchakato wa kuwatafutia sehemu nyingine unaweza kuwa changamoto kwao kufikia malengo waliyojiwekea.

Tanzania haitakuwa nchi ya kwanza Afrika kuwa na mji wa unaowaweka wabunifu wa teknolojia pamoja, Afrika Kusini wana eneo la Braamfontein katika Jiji la Johannesburg na Silicon Cape jijini Cape Town.

 

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
19 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
19 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
19 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Siku ya Familia, Mtoto wa Afrika kuadhimishwa Juni 30, 2026

Siku ya Familia, Mtoto wa Afrika kuadhimishwa Juni 30, 2026

Nukta TV

Wadau wa 'kubet" watoa ya moyoni, pendekezo kupanda kwa tozo 5%

Wadau wa 'kubet" watoa ya moyoni, pendekezo kupanda kwa tozo 5%

Nukta TV

Wasemayo wananchi, vocha za kukwangua kupigwa maruku mijini

Wasemayo wananchi, vocha za kukwangua kupigwa maruku mijini

Nukta TV