Vodacom Tanzania, WWF kuifanya Dodoma kuwa ya kijani kwa Sh303 milioni

August 21, 2019 5:23 am · Daniel
Share
Tweet
Copy Link
  • Wanakusudia kutekeleza mradi wa upandaji miti ili kulifanya Jiji la Dodoma kuwa la Kijani na kuwainua kiuchumi vijana na wanawake. 
  • Watapanda miti zaidi ya laki 100,000 na kutengeza bustani ya kupumzikia karibu na  Chuo Cha Elimu ya Biashara (CBE) kampasi ya Dodoma. 
  • Vijana na wanawake watapewa ujuzi wa kutengeneza mifuko mbadala ili kujikwamua kiuchumi. 

Dar es Salaam. Kampuni ya simu ya Vodacom Tanzania imesaini mkataba wa makubaliano na Mfuko wa Uhifadhi wa Wanyama pori (WWF) kwa ajili ya kuchangia Sh303 milioni zitakozotumika katika mradi wa upandaji miti na kutengeneza ajira kwa vijana na wanawake wa Jiji la Dodoma. 

Mkubaliano hayo yakuifanya Dodoma kuwa ya kijani yamefikiwa leo (Agosti 20, 2019) jijini Dar es Salaam, ikiwa ni mradi wa mwaka mmoja utakaotekelezwa kwa kushirikiana na Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Halmashauri ya Jiji la Dodoma na Taasisi ya Huduma za Misitu (TSF).

Malengo mengine  ya mradi huo ni kuwainua vijana na  wanawake kupitia miradi wezeshi ikiwemo ya kutengeza mifuko ya mbadala kwa kutumia teknolojia rahisi. 

Vodacom Tanzania imeingia makubaliano hayo kupitia taasisi yake ya Vodacom Tanzania Foundation  ambapo itachangia Sh303 milioni kwa ajili mradi huo uliopewa jina la “Kuishi kwa furaha na maliasili”.

Mratibu wa mradi huo, Savinuss Kessy amesema mradi huo wa kuifanya Dodoma kuwa ya kijani utaanza Septemba mwaka huu hadi Machi 2020 katika kilele cha siku ya “Earth Hour” huko Dodoma.

“Mradi huo utajumuisha upandaji wa miti ipatayo 100,000 katika maeneo ya mji wa Serikali wa  Mtumba na Chamwino ambapo Ikulu ipo pamoja na barabara za mji wa Dodoma na zinazoingia katika ya mji huo,” amesema Kessy.

Kessy amesema pia mradi utasaidia kuwapa ujuzi vijana na akina mama jinsi ya kutengeza mifuko mbadala ikiwa ni njia mojawapo ya kuendelea kukuza ajira kwa njia ya kujiajiri. 


Zinazohusiana: 


Akizungumza katika halfa hiyo, Dk Thomas Bwana ambaye alikuwa mgeni rasmi kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais amesifu makubaliano hayo kati ya Vodacom Tanzania na WWF katika jitihada zao za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

“Nimefurahi namna makampuni na mshirika yasiyokuwa ya kiserikali yanavyoungana kufanikisha Malengo ya Maendeleo Endelevu namba 13 juu ya hali ya hewa,” amesema Dk Bwana.

Pia makubaliano hayo yatasaidia kujengwa kwa bustani ya kupumzikia karibia na Chuo Cha Elimu ya Biashara (CBE) kampasi ya Dodoma. 

Mkurugenzi  wa Vodacom Tanzania Foundation, Rosalynn Mweria amesema wamefurahi kuingia ubia na WWF ili kutekeleza mpango huo ambao unawiana na mpango mkakati wa Vodacom Tanzania kwa mwaka 2019/2021.

Naye Mkurugezi Mkazi wa WWF Tanzania , Dk Amani Ngusaru ameishukuru Vodacom Tanzania Foundation  kwa kuunga mkono mradi huo na amesema mfuko huo unaunga juhudi za Serikali katika kuufanya mji wa Dodoma kuwa wa kijani na kwa mwaka wa kwanza watapanda miti laki 100,000.

Dk Ngusara amesema mradi huo utaongeza ufahamu na kuhamisisha  jamii kushiriki programu rafiki za ikolojia kwa kuwapa mafunzo makundi ya vijana na wanawake katika uzalishaji na matumizi ya mifuko mbadala na kusimamia taka katika kuzifanya kuwa shughuli wezeshi ya kiuchumi.

Follow Us on TikTok

FOLLOW NOW

Subscribe to Our YouTube Channel

SUBSCRIBE NOW