Vipaumbele vinne vya bajeti ya Serikali 2020-2021

June 11, 2020 11:04 am · TULINAGWE ALSON
Share
Tweet
Copy Link
  • Baadhi ya vipaumbele hivyo ni pamoja na ujenzi wa msingi wa uchumi wa viwanda na kufungamanisha uchumi na maendeleo ya watu. 
  • Uboreshaji wa mazingira wezeshi kwa uendeshaji wa biashara na uwekezaji nchini Tanzania.

Dar es Salaam. Serikali imesema katika mwaka wa fedha wa 2020/21 itatekeleza maeneo manne ya vipaumbele ikiwemo ujenzi wa viwanda vya kukuza uchumi wa Taifa na kuboresha maisha ya Watanzania. 

Waziri wa fedha na mipango, Dk Philip Mpango amesema maeneo hayo ya miradi na shughuli za kipaumbele kwa mwaka 2020/21 ni mwendelezo wa kutekeleza Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2016/17 – 2020/21. 

Amesema kipaumbele cha kwanza ni viwanda vya kukuza uchumi na ujenzi wa msingi wa uchumi wa viwanda ambapo serikali itajikita zaidi katika uendelezaji na ujenzi wa viwanda vinavyotumia malighafi zinazopatikana kwa wingi nchini. 

Serikali itafungamanisha ukuaji wa uchumi na maendeleo ya watu kwa kuendeleza huduma za kijamii ikiwemo elimu, afya na upatikanaji wa maji sa na salama kwa Watanzania.

“Tutaendelea kusomesha kwa wingi wataalamu kwenye fani na ujuzi adimu kama vile udaktari, mafuta na gesi, Jiolojia, Jemolojia na Uhandisi migodi; kuendelea kugharamia utoaji wa elimumsingi bila ada,” amesema Dk Mpango. 

Uboreshaji wa mazingira wezeshi kwa uendeshaji uiashara na wekezaji ambapo miradi itakayotekelezwa katika eneo hili italenga kuendeleza ujenzi na ukarabati wa miundombinu wezeshi ili kurahisisha uendeshaji biashara na uwekezaji nchini. 

“Miradi hiyo ni pamoja na kuendelea na ujenzi wa reli ya kati katika kiwango cha kimataifa cha standard gauge(kiwango cha kisasa), kuendelea na ukarabati wa vichwa vya treni, mabehewa ya mizigo na abiria pamoja na njia za reli ya kati na TAZARA,” amesema Waziri huyo akianisha kipaumbele cha tatu. 


Zinazohusiana:


Kuimarisha usimamizi wa utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo kwa mwaka 2020/21 ambapo miradi itakayotekelezwa inalenga kuimarisha mifumo na taasisi za utekelezaji na usimamizi wa Mpango, kuongeza upatikanaji wa rasilimali fedha za kutekeleza mpango na kuweka vigezo vya upimaji wa matokeo ya utekelezaji. 

Amesema miradi hiyo itajumuisha maeneo ya utawala bora hususan utoaji haki na huduma za kisheria, kuimarisha miundombinu ya mahakama, bunge na vyombo vya ulinzi na usalama.

Aidha, Serikali imesema mpango huo utazingatia umuhimu wa kuimarisha Muungano wa Tanzania bara na Zanibar kwa usimamizi wa shughuli za uvuvi, kuboresha programu za mabadiliko ya tabianchi na mpango wa kunusuru kaya maskini.

“Katika mwaka 2020/21, msukumo mkubwa utawekwa katika kukamilisha utekelezaji wa miradi inayoendelea ili kupata matokeo tarajiwa,” amesema Dk Mpango.

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: RAIS SAMIA ANAZINDUA MELI YA KWANZA YA UVUVI WA BAHARI KUU

🔴LIVE: RAIS SAMIA ANAZINDUA MELI YA KWANZA YA UVUVI WA BAHARI KUU

Nukta TV

Kwa nini wanawake wako katika hatari zaidi kupata magonjwa ya akili?

Kwa nini wanawake wako katika hatari zaidi kupata magonjwa ya akili?

Nukta TV

🔴LIVE: HOMERA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA BUNGENI

🔴LIVE: HOMERA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA BUNGENI

Nukta TV

BENEFIT FROM
Nukta ADS
Advertise with us to reach a wider audience with high conversion rates.
Other Nukta Africa Products
Nukta Habari
Stories that matter
Topics
Inuldge yourself with the topics in Nukta
All
Business
Africa
Contact
Tel
+255 750 881 888
Mail
newsroom@nukta.co.tz
Address
Mwananyamala kwa Kopa Dabe House Dar es Salaam TZ, 14108
Social Media

© 2024 Nukta Africa. All Rights Reserved.