Utoaji mikopo ya halmashauri wasitishwa kwa siku 30

April 26, 2022 9:45 am · Mariam John
Share
Tweet
Copy Link
  • Mkoa wa Mwanza wasitisha zoezi hilo baada ya kubaini madudu.
  • Wapo waliopata mikopo bila sifa, wengine washindwa kurudisha.
  • Watumishi waliohusika katika hujuma kikaangoni. 

Mwanza. Serikali mkoani Mwanza imesitisha utoaji wa fedha za mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na halmashauri ndani ya siku 30 ili kupisha uchunguzi baada ya kuwepo kwa ukiukwaji mkubwa wa utolewaji wa fedha hizo kinyume cha kanuni na sheria za mikopo hiyo.

Mkuu wa Mkoa, Mhandisi Robert Gabriel katika taarifa yake kwa waandishi wa habari jana Aprili 25, 2022 ilibainisha kuwepo kwa mapungufu 12 yaliyokiukwa wakati wa utolewaji wa fedha hizo katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita (2019 hadi 2021) na kusababisha upotevu wa fedha nyingi za Serikali.

“Tumesitisha utoaji wa fedha hizo ndani ya siku 30 ili kupisha uchunguzi kwa kamati zinazohusika na utoaji wa mikopo lakini pia kufanya ufuatiliaji wa kina wa fedha zilizotolewa ili wale waliochukua kinyume na taratibu wazirudishe,” amesema Gabriel.

Mhandisi Gabriel akibainisha mapungufu hayo, amesema kufuatia tume aliyoiunda kuchunguza utolewaji wa mikopo hiyo ilibaini wapo watumishi wa umma na wenye ajira walibainika kuchukua fedha hizo kinyume cha sheria na kanuni za utoaji wa mikopo na pia ilibaini kuwepo kwa vikundi hewa zaidi ya 34.

Tume hiyo pia ilibaini uidhinishwaji wa fedha bila nyaraka za mwenyekiti wa serikali ya mtaa na mtendaji wa eneo husika, vikundi kukosa uthibitishwaji, vikundi kushindwa kurejesha fedha kwa kipindi husika na kamati ya utoaji wa mikopo kushindwa kutoa matangazo.


Soma zaidi:


Mapungufu mengine ni uwepo wa vikundi ambavyo vilichukua fedha  bila kukamilisha mikopo ya awali, vingine vilichukua fedha bila kutia saini, vikundi vingine vilipata mikopo hiyo bila maombi ya mikopo kupitia kwenye vikao.

“Tunatoa rai kwa watumishi wa umma waliochukua fedha hizo kuzirudisha mara moja ili vikudi vingine vinavyokidhi matakwa viweze kuchukua fedha hizo.

“Tayari Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) ipo kazini kuchunguza. Pia Jeshi la Polisi nao wapo kazini kufuatilia mienendo yote ya utolewaji wa fedha hizo ili wale waliokiuka wachukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria,” amesema Mhandisi Gabriel.

Amesema fedha hizo ni za serikali na haziwezi kupotea, hataonewa mtu na mkoa hawatakubali kuona fedha ya serikali ikichezewa. 

“Lengo ni kurudisha nidhamu ya usimamizi wa mali ya umma na zaidi kuwa na  huruma kwa vijana ambao wana kiu ya kubadilisha maisha yao kupitia fedha hizo,” amesisitiza.

Amewataka wale waliochukua fedha hizo na kwenda kuzigawa wajiorodheshe na kuzirudisha mapema na kwa utaratibu.

Katika kipindi hicho cha miaka mitatu, Mkoa wa Mwanza ulitoa zaidi ya Sh8.778 bilioni kwenye vikundi vya wajasiriamali wadogo na hadi kufikia mwezi Februari mwaka huu nusu ya fedha hiyo ilikuwa haijarejeshwa.

Mwaka jana, Nukta Habari, alitoa ripoti maalum inayoonyesha mwenendo usirodhisha wa utoaji mikopo hiyo katika mkoa huo ambapo kulikuwa na malalamiko kuwa inatolewa kwa upendeleo na itikadi za vyama huku baadhi ya watumishi wakidai rushwa kuwapatia wahusika.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jul, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Kutana na ‘Poultry Plucker’, mashine inayonyonyoa kuku watatu kwa dakika moja

Kutana na ‘Poultry Plucker’, mashine inayonyonyoa kuku watatu kwa dakika moja

Nukta TV

Rais Samia: Kalamu yangu ina hatari, sijawahi kusaini mtu kunyongwa

Rais Samia: Kalamu yangu ina hatari, sijawahi kusaini mtu kunyongwa

Nukta TV

Rais Samia: Matumizi jina Samia, likiwa kila mahali inachosha, tafuteni wengine

Rais Samia: Matumizi jina Samia, likiwa kila mahali inachosha, tafuteni wengine

Nukta TV