Usuluhishi unavyoweza kupunguza mrundikano wa kesi mahakamani

January 23, 2023 12:03 pm · Mariam John
Share
Tweet
Copy Link

Iwapo wananchi watatumia njia hiyo watasaidia kupunguza mrundikano wa kesi mahakamani na kwamba watumie wazee wenye busara walioko kwenye maeneo yao  kuhakikisha wanatatua changamoto hiyo. Picha | Mariam John.


  • Ni kwa wadawa meza moja kabla ya kukimbilia mahakamani.
  • Hiyo inasaidia kupunguza chuki kati ya ndugu na marafiki. 

Mwanza. Jamii imetakiwa kutatua migogoro yao kwa njia ya usuluhishi kuliko kukimbilia mahakamani ili kuepuka chuki na kisasa kinachoweza kutokea kwa upande mmoja utakaonyimwa haki.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, Dk Ntemi Majenga akizungumza kwenye uzinduzi wa wiki ya sheria jijini Mwanza Januari 23, 2022 amesema jamii inapotatua migogoro yao kwa njia ya usuluhishi inategengeneza mambo makuu mawili moja ni wananchi wanabaki kuwa marafiki.

“Wanaendelea kuwa marafiki kwa maana ya kula pamoja, kuzungumza na kushirikiana kwenye shughuli mbalimbali za kijamii, suala lingine ni kuwa wadaiwa wao ndio wanakuwa waamuzi wa utatuzi wa mgogoro huo huku mahakama ikibakia kuandika kile ambacho wamekubaliana,” amesema Dk Majenga.

Mathalan, watu wanagombani shamba, amesema hiyo si kesi ya kufikishana mahakamani ni suala la kukubaliana na kuamua wao na kila mmoja akabaki na amani, hiyo itasaidia kuokoa muda na gharama zingine.

Amesema ipo changamoto ambapo wananchi wanapokuwa na mgogoro wanakimbilia mahakamani hata kama kesi ilikuwa ni ndogo ambayo wangeimaliza wao wenyewe na wakaendelea kuwa marafiki.

“Ndio maana kama mahakama tukaona kwamba si lazima sana migogoro inapotokea ipelekwe mahakamani kwani umuhimu wa kutatua migogoro kwa njia ya usuluhishi itasaidia kuleta amani na itaondoa chuki,” amesema Dk Majenga.

Dk Majenga amesema iwapo wananchi watatumia njia hiyo watasaidia kupunguza mrundikano wa kesi mahakamani na kwamba watumie wazee wenye busara walioko kwenye maeneo yao  kuhakikisha wanatatua changamoto hiyo.

Salum Kali, Mkuu wa Wilaya ya Magu kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Adam Malima amesema njia hiyo ya kutatua migogoro kwa usuluhishi itapunguza migogoro ya ardhi.

Kali amesema bado kuna migogoro mingi ikiwemo ya ardhi, ndoa, mirathi, ajira na biashara na kwamba watu wengi wanatumia muda mwingi na fedha kutatua migogoro hiyo badala wangeitatua kwa usuluhishi na kuendelea na shughuli nyingine za uzalishaji.

“Migogoro mingi ni hasara kwa sababu inamlazimu mtu atumie rasilimali nyingi za fedha na muda hasa pale mmoja anapotangazwa mshindi na mwingine kushindwa, hivyo ni vizuri iwapo ingefanyika kwa usuluhishi ili kila mmoja kuondoka akiwa na amani,” amesema Kali.

Baadhi ya wananchi wamesema uamuzi ulioletwa na mahakama unaweza kuwa mzuri lakini wapo baadhi ya watu hupenda kuwagandamiza wanyonge.

Husna Athuman anasema hiyo itasaidi kupunguza mrundikano wa kesi mahakamani lakini pia ni vyema elimu ikatolewa ili wananchi waweze kuelewa kwakuwa wapo wengine hutumia mali zao kugandamiza wengine.

Kauli mbiu ya mwaka huu ya Wiki ya Sheria ni umuhimu wa utatuzi wa migogoro kwa njia ya usuluhishi katika kukuza uchumi endelevu wajibu wa mahakama na wadau.

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
PART 2: Yafahamu magari 10 yanayotumia kiwango kidogo cha mafuta.

PART 2: Yafahamu magari 10 yanayotumia kiwango kidogo cha mafuta.

Nukta TV

🔴LIVE: LIVE:WABUNGE WAKIWACHAPA MASWALI MAWAZIRI | Bunge la 13 | Kikao cha 28

🔴LIVE: LIVE:WABUNGE WAKIWACHAPA MASWALI MAWAZIRI | Bunge la 13 | Kikao cha 28

Nukta TV

PART 1: Yafahamu magari 10 yanayotumia kiwango kidogo cha mafuta

PART 1: Yafahamu magari 10 yanayotumia kiwango kidogo cha mafuta

Nukta TV