Unywaji wa maziwa bado bado Tanzania

May 28, 2024 3:37 pm · Mariam John
Share
Tweet
Copy Link
  • Mwenyekiti wa DTB asema kiwango kidogo cha unywaji wa maziwa husababisha udumavu kwa watoto.
  • Awataka wachakataji maziwa kusogeza huduma hiyo karibu na wananchi.

Mwanza: Mwenyekiti wa Bodi ya Maziwa (DTB), Zacharia Masanyiwa  amesema unywaji wa maziwa bado ni tatizo kwa watu wengi nchini jambo linalosababisha  baadhi yao ikiwemo watoto kukosa virutubisho muhimu vinavyojenga mwili.

Masanyiwa aliyekuwa akitembelea kiwanda cha uchakataji wa maziwa kilichopo Mecco mkoani Mwanza leo Mei 28, 2024 amesema bodi hiyo ni miongoni mwa wadau muhimu katika kuhamasisha unywaji wa maziwa nchini ili kukabliana na udumavu.

“Bodi ya Maziwa ni miongoni mwa wadau muhimu katika sekta ya afya kwa kuhamasisha unywaji wa maziwa ili kukabiliaiana na tatizo la udumavu kwa watoto nchini,” amesema Masanyiwa.


Soma zaidi: Ifahamu mikoa 10 inayoongoza kwa uzazi wa mpango Tanzania


Kauli hiyo ya Masanyiwa inakuja wakakati Tanzania ikiadhimisha wiki ya maziwa iliyoanza leo na kilele chake kitafanyika Juni Mosi, 2024 jijini Mwanza.

Bodi hiyo imetumia wiki ya maziwa kugawa kinywaji hicho katika Hospitali ya Nyamagana na kituo cha kuelelea watoto cha Hope village kilichopo mkoani Mwanza ambapo pia imeagiza  wachakataji wa maziwa kuweka dirisha maalum  la kuuza kiywaji hicho maeneo ya hospitali ili kuongeza hamasa ya unywaji wa maziwa kwa wananchi.

Baadhi ya wakazi jijini Mwanza wameeleza sababu zinazochangia wao kutokunywa maziwa ni ukosefu wa fedha kwa kuwa maziwa yanauzwa ghali na hayapatikani kirahisi.

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Kwanini uchafuzi wa mazingira ni tishio kwa afya ya binadamu na uchumi

Kwanini uchafuzi wa mazingira ni tishio kwa afya ya binadamu na uchumi

Nukta TV

Tunachokifahamu kuhusu ziara ya Rais Samia Urusi, kidiplomasia na uchumi

Tunachokifahamu kuhusu ziara ya Rais Samia Urusi, kidiplomasia na uchumi

Nukta TV

Kutoka Ubunge hadi mshauri wa Rais, Panda shuka ya Ummy Mwalimu katika siasa

Kutoka Ubunge hadi mshauri wa Rais, Panda shuka ya Ummy Mwalimu katika siasa

Nukta TV