Trace Together: App iliyobuniwa kupambana na Corona

March 23, 2020 9:59 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link

Muonekano wa app wa TraceTogether inayosaidia kupata taarifa za corona. Picha|Mtandao.


  • Imezindua programu tumishi ya simu (app)  itakayowezesha Serikali kuwafuatilia na kuwatambua watu waliokaribiana na wagonjwa wa maradhi ya COVID-19 kama moja ya juhudi za kukabiliana na kusambaa kwa virusi vya corona. 

Wakati wanasayansi duniani wakiendelea kutafuta tiba na chanjo ya ugonjwa virusi vya Corona (COVID-19), wabunifu nao wanabuni mifumo ya kidijitali itakayosaidia kuongeza ufanisi wa tahadhari za kujikinga na ugonjwa huo unaosambaa kwa kasi duniani. 

Nchi ya Singapore imezindua programu tumishi ya simu (app)  itakayowezesha Serikali kuwafuatilia na kuwatambua watu waliokaribiana na wagonjwa wa maradhi ya COVID-19 kama moja ya juhudi za kukabiliana na kusambaa kwa virusi vya corona. 

App hiyo iliyopewa jina la TraceTogether app, ilizinduliwa jana (Machi 20, 2020) na shirika la teknolojia la serikali ya Singapore la GovTech kwa kushirikiana na wizara ya afya ambapo inaweza kupakuliwa na wananchi wa Singapore wenye namba za simu na simu janja zenye “Bluetooth”.

App hiyo itakuwa inabadilishana taarifa za watu wanaopishana barabarani kwa umbali usiozidi mita mbili kupitia bluetooth ili kutambua taarifa za mtu mwingine. 


Soma zaidi: 


Rekodi zao zitatunzwa kwenye app iliyoko kwenye simu na hazitatumwa kwa mamlaka husika. 

Watumiaji watatakiwa kutuma taarifa zao ikiwa wataombwa na Wizara ya Afya ikiwa ni sehemu ya uchunguzi wa kufuatilia ukaribu wa watu. Ikiwa mtu atakataa kubadilishana taarifa na wizara anaweza kushitakiwa chini ya Sheria ya Magonjwa ya Yanayoambukiza ya nchi hiyo.  

Ingawa hakuna atakayelazimishwa kuwa na app hiyo, Serikali imesema itawahamasisha watu kuwa nayo.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwenendo wa deni la serikali

Mwenendo wa deni la serikali

Nukta TV

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Nukta TV

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Nukta TV