Teleza, uliwe: Ushindani mkali huduma za intaneti Tanzania
- Kampuni ya Vodacom Tanzania inatoza Sh98 kwa MB 1 ya intaneti ukifuatiwa na Zantel.
- Tozo hizo ni kwa watumiaji wa simu janja ambao hawajiungi na vifurushi vya intaneti wanapokuwa mtandaoni.Â
- Smile ndiyo kampuni inayotoza viwango vya chini kabisa vya intaneti.
Dar es Salaam. Licha ya kampuni ya simu ya Vodacom Tanzania kushusha gharama za intaneti nje ya bando (vifurushi) bado mtandao huo umeendelea kuwa ghali zaidi ukilinganisha na kampuni nyingine nchini Tanzania.Â
Gharama hizo huusisha tozo ambazo watumiaji wa intaneti hukatwa kwenye vocha zao za simu wakati wanatumia huduma hiyo pasipo kujiunga na virushi vya intaneti.Â
Ripoti mpya ya mawasiliano Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ya robo ya kwanza ya mwaka 2020 inaonyesha kuwa Vodacom inawatoza wateja wake Sh98 kwa kila megabaiti 1 (MB) kabla ya kodi ikiwa ni ahueni kutoka Sh150 kwa MB katika robo ya mwisho ya mwaka 2019.Â
Hiyo ni sawa na kusema kama mtumiaji wa simu janja atakayeweka vocha ya Sh500 na akaruhusu intaneti itumike bila kujiunga na kifurushi cha intaneti, basi atapata MB5.10 Â kabla ya kodi kwa tozo hizo mpya za Vodacom.Â
Tozo hizo zimepungua kutoka Sh150 iliyokuwa inatozwa katika robo ya nne ya mwaka 2019, jambo linalowapa ahueni watumiaji wa intaneti ya Vodacom kwa kuokoa Sh52 kwa kila MB1. Â
Tozo hizo zinazotozwa na kampuni za mawasiliano kwenye intaneti hazijumuishi kodi ya Serikali (Tax Exclusive).
Hata hivyo, tozo za intaneti za Vodacom ni kubwa zaidi ya zile zinavyotozwa na kampuni nyingine za simu nchini ambazo tozo zake hazizidi Sh50 kwa MB1
Takwimu hizo za TCRA za kati ya Januari na Machi 2020 zinaonyesha kuwa mteja wa Vodacom anayetumia intaneti kwa vocha ya simu yake bila kifurushi anatozwa zaidi ya mara 16 ya yule wa Smile ambaye mtandao wake unamtoza Sh6 kwa MB1.
Soma zaidi:
Smile ndiyo mtandao wenye kiwango cha chini cha tozo za intaneti kwa wateja wake  miongoni mwa kampuni za simu Tanzania.Â
Mtandao ambao unafuata kwa viwango vikubwa vya tozo za intaneti baada ya Vodacom ni Zantel ambao unakata Sh41 kwa MB1 ikifuatiwa na Tigo na Airtel ambazo zote zinatoza Sh40.
Halotel wao wanatoza Sh26 kwa MB1 huku TTCL ambayo inamilikiwa na Serikali inawatoza watumiaji wake Sh14 kwa MB1 ikiwa wataweka vocha na kuruhusu intaneti itumike katika simu zao bila vifurushi.Â
Pamoja na kutoza kiwango cha juu nje ya kifurushi, Vodacom ni miongoni mwa mitandao inayotoza bei ya chini intaneti ya vifurushi ambapo hutoza Sh5 kwa kila MB1 ikijumuisha na kodi.Â
Kiwango hicho cha Vodacom ni pungufu zaidi ya mara saba ya kile kinachotozwa na Airtel cha Sh37 ambacho ni cha juu kabisa miongoni mwa kampuni za mawasiliano nchini.Â
Airtel inafuatiwa na Tigo ambayo hutoza Sh23 huku TTCL ndiyo mtandao pekee unaotoza kiwango cha chini cha Sh0.7.Â
Huduma ya intaneti kwa njia ya simu (mobile internet) imekuwa ni biashara ambayo inazipatia faida kubwa kampuni za simu, ikizingatiwa kuwa watu wengi wenye simu janja wanatumia intaneti kuperuzi vitu mbalimbali mtandaoni.Â
Mathalan, ripoti ya awali ya kifedha ya Vodacom Tanzania ya mwaka unaoishia Machi 2020 inaonyesha watumiaji wa intaneti ya kampuni hiyo katika kipindi hicho walifikia milioni 7.7 huku mapato ya huduma hiyo yaliongezeka kwa asilimia 9.8 hadi Sh180.8 bilioni.Â