TCRA yaifungia Jamii Forums kwa siku 90

September 6, 2025 3:31 pm · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni kutokana na kuchapisha maudhui kinyume na sheria.

Arusha. Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imesitisha leseni ya kuchapisha maudhui mtandaoni ya kampuni ya Vapper Tech Limited (JamiiForums) na kuzuia upatikanaji wa jukwaa la Jamii Forums kwa siku 90.

Taarifa ya Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Dk Jabiri Bakari, iliyotolewa leo Septemba 9, 2025 inabainisha kuwa leseni hiyo imesitishwa kutokana na kuchapisha maudhui kinyume na sheria bila kubainisha maudhui yenyewe.

“Mnamo tarehe 04 Septemba 2025, Jamii Forums kupitia jukwaa lake na akaunti zake za mitandao ya kijamii ilichapisha maudhui ya kupotosha Umma, kukashifu na kudhalilisha Serikali na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kinyume na Kanuni za Maudhui Mtandaoni za mwaka 2020 na Marekebisho yake ya mwaka 2022 па 2025,” imesema taarifa ya Dk Bakari.

TCRA imebainisha kuwa maudhui hayo pia yanakinzana na utamaduni, mila na desturi za Kitanzania, jambo ambalo linaathiri umoja, amani na mshikamano wa kitaifa, na kuharibu taswira ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hata hivyo, kwa mujibu wa Jamii Forums  uamuzi wa TCRA  umetokana na wao kuchapisha taarifa ya mwanasiasa Humphrey Polepole kuhusu mfanyabiashara Rostam kumiliki mgodi wa makaa ya mawe kwa asilimia 70 na taarifa za uhusiano kati ya Rais wa Tanzania na mfanyabiashara raia wa Zimbabwe Wicknell Chivayo bila kuzingatia mizania.

“Jamii Forums ilishindwa kutafuta maoni ya Mamlaka husika/Msemaji wa Rais/Serikali, kuthibitisha uhalisia wa picha (za Rais na Chivayo) zilizotumika, na hivyo kuuaminisha Umma taarifa za upande mmoja,” imesema taarifa ya Jamii Forums ikinukuu maamuzi ya TCRA.

Kwa hukumu hiyo Jamii Forums pamoja na majukwaa yake yote ya mtandaoni haitaweza kurusha taarifa za uchaguzi unaotarajia kufanyika Oktoba 29, mwaka huu kama ambavyo imekuwa ikifanya miaka.ya nyuma kwa kuwa itakuwa ndani ya kipindi cha adhabu.

Hii si mara ya kwanza kwa TCRA kufungia chombo cha habari Tanzania.

Oktoba 2024 TCRA ilisitisha  leseni zote za kuchapisha maudhui mtandaoni za kampuni ya Mwananchi Communication Ltd kwa kwa tuhuma za kuchapisha maudhui yaliyokiuka Sheria za nchi na kuleta tafsiri hasi kwa Taifa.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
19 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
19 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
19 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Siku ya Familia, Mtoto wa Afrika kuadhimishwa Juni 30, 2026

Siku ya Familia, Mtoto wa Afrika kuadhimishwa Juni 30, 2026

Nukta TV

Wadau wa 'kubet" watoa ya moyoni, pendekezo kupanda kwa tozo 5%

Wadau wa 'kubet" watoa ya moyoni, pendekezo kupanda kwa tozo 5%

Nukta TV

Wasemayo wananchi, vocha za kukwangua kupigwa maruku mijini

Wasemayo wananchi, vocha za kukwangua kupigwa maruku mijini

Nukta TV