Tanzania, Singapore zasaini makubaliano kuimarisha biashara na uwekezaji

June 9, 2026 4:50 pm · Kelvin Makwinya
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni kufuatia ziara ya Rais wa Singapore nchini ambayo ni kwa mara ya kwanza tangu mataifa haya kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia miaka 45 iliyopita.

Dar es Salaam. Serikali ya Tanzania imesaini mikataba ya ushirikiano na Serikali ya Singapore yenye lengo la kuimarisha biashara, uwekezaji na kukuza tija ya kiuchumi kati ya mataifa hayo mawili.

Rais wa Samia Suluhu Hassan aliyekuwa akizungumza mara baada ya mazungumzo rasmi na Rais wa Singapore, Tharman Shanmugaratnam, aliyewasili nchini jana kwa ziara ya kikazi ya siku tatu,  amesema kuwa uhusiano wa kibiashara uliopo kwa sasa bado hauendani na kiwango cha urafiki na ushirikiano wa muda mrefu kati ya nchi hizo.

“Biashara kati yetu ni Dola za Marekani milioni 299, na uwekezaji ni miradi 36 ya Singapore ndiyo iko hapa nchini, na hii haihakisi kiwango cha urafiki wetu,” amesema Rais Samia.

Kwa upande wake, Rais wa Singapore, Tharman Shanmugaratnam amesema Tanzania imejijengea taswira nzuri kimataifa kutokana na uwezo wake wa kiuchumi na nafasi yake ya kimkakati katika ukanda wa Afrika Mashariki, akisisitiza haja ya kuimarisha zaidi ushirikiano huo.

“Tanzania tayari imeacha taswira nzuri na ya kuvutia, ikiwa ni nchi iliyojiamini katika uwezo wake na iliyopo katika nafasi nzuri ya kunufaika na fursa zilizopo. Mwaka huu tumeadhimisha miaka 45 ya uhusiano wa kidiplomasia, na kama nilizungumza na Rais asubuhi hii kwamba ni wakati muafaka wa kuingiza kasi mpya katika uhusiano wetu na kuchunguza maeneo mapya ya ushirikiano wa vitendo,” amesema Rais Shanmugaratnam.

Ziara hiyo ya Rais Shanmugaratnam ni ya kwanza kwa kiongozi wa ngazi ya juu kutoka Singapore kufanya ziara nchini Tanzania tangu mataifa hayo mawili kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia mwaka 1980.

Rais Shanmugaratnam anatarajia kumaliza ziara yake hapo kesho Juni 10, 2026 ambapo pamoja na mambo mengine, atafanya mazungumzo na Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi, kuhusu maeneo ya ushirikiano yenye maslahi ya pamoja hususan katika sekta za uchumi wa buluu, utalii na uwekezaji.

Mbali na hayo, Rais Samia ambaye ametoka kufanya ziara ya kikazi nchini Urusi, ameitaka Singapore kufungua ubalozi wake hapa nchini Tanzania ili kuimarisha zaidi uhusiano wa kidiplomasia na kiuchumi kati ya pande hizo mbili.

Huenda sasa dilomasia ya Tanzania inaimarika kwa kasi kwani katika kipindi kifupi tangu mwaka huu kuanza zaidi ya marais wanne wamezuru Tanzania kwa ziara za kikazi ikiwemo, Yoweri Museveni wa Uganda, Paul Kagame wa Rwanda na William Ruto wa Kenya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mikakati ya Serikali kuhakikisha walimu wa VETA wanapata ajira na mikopo

Mikakati ya Serikali kuhakikisha walimu wa VETA wanapata ajira na mikopo

Nukta TV

Mama Salama alivyombana Wanu kuhusu maslahi ya walimu wanaojitolea

Mama Salama alivyombana Wanu kuhusu maslahi ya walimu wanaojitolea

Nukta TV

Kwanini uchafuzi wa mazingira ni tishio kwa afya ya binadamu na uchumi

Kwanini uchafuzi wa mazingira ni tishio kwa afya ya binadamu na uchumi

Nukta TV