Tanzania bado bado kurejea Mahakama ya Haki Afrika Mashariki
Rais Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi pamoja na Wajumbe wa Chama cha Wanasheria wa Afrika Mashariki (East Africa Law Society) kabla ya kufungua Mkutano wa 27 wa Chama hicho uliofanyika Jijini Arusha Novemba 24, 2022. Picha | Ikulu.
- Rais Samia ataka pande zote mbili zijitafakari kwanza kabla ya kurejea.
- Tanzania ilijitoa mwaka 2020.
Dar es salaam. Rais Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania inahitaji muda zaidi wa kutafakari na kurekebisha baadhi ya mambo kabla haijarejea katika Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (AfCHPR).
Itakumbukwa Novemba 26, 2020 Tanzania ilijiondoa rasmi kwenye kipengele cha AfCHPR kinachoruhusu watu binafsi na mashirika yasiyo ya kiserikali kuishtaki Serikali.
Uamuzi huo uliopingwa vikali na baadhi ya wadau wa sheria na mashirika ya kutetea haki za binadamu ulitokana na kusudio la kujitoa katika ibara ya 34 kifungu cha (6) ya mahakama ya AfCHPR, ambalo liliwasilishwa na Serikali ya Tanzania Novemba 21, 2020.
Rais Samia aliyekuwa akihutubia katika ufunguzi wa mkutano wa 27 wa Jumuiya ya Wanasheria Afrika Mashariki leo Novemba 24, 2022 amesema amepokea ombi la kurejeshwa kwa kifungu hicho lakini mpaka baadhi ya mambo yatakapofanyiwa kazi.
“Kati ya kesi 360 zilizopelekwa kwenye mahakama hiyo zaidi ya kesi 260 zilikuwa dhidi ya Serikali ya Tanzania, hivyo tulijitoa ili wao wajirekebishe kwao na sisi tujirekebishe kwetu kisha tutarejea kwenye mashirikiano,” amesema Rais Samia.
Rais Samia amesisitiza kuwa ni muhimu kwa kila upande kutafakari kwa kina nini kinaweza kufanyika ili kurudisha ushirikiano uliokuwepo awali.
Soma zaidi:
Licha ya kujiondoa katika kifungu hicho bado Tanzania ni mwanachama wa mahakama hiyo iliyopo jijini Arusha kutokana na kuendelea kuheshimu kipengele cha mwongozo wa uanzishwaji wa mahakama hiyo.
Aidha Samia ametumia mkutano huo kuwaasa wanasheria kutenda haki katika utekelezaji wa majukumu yao pamoja na kuimarisha ushirikiano baina yao hususan katika kesi za kimataifa ili kuongeza ujuzi na weledi.
Latest