“Startup” iliyowekeza kupanda miti yapokea Sh64.9 bilioni Kenya
Hadi sasa, Komaza imeshirikiana na wakulima zaidi ya 6,000 ambapo kwa kipindi chote tangu kuanzishwa kwake, imepanda miti milioni 2. Picha| Barr Foundation.
- Ni startup inayojihusisha na upandaji wa miti na kutoa elimu kwa wakulima.
- Start up hiyo imedhamilia kupanda miti bilioni moja ifikapo mwaka 2030.
- Hadi sasa, ikishirikiana na wakulima nchini Kenya, imepanda miti milioni 2.
Dar es Salaam. Kampuni inayochipukia ya Komaza ya nchini Kenya imepigwa jeki ya Sh64.9 bilioni kuiwezeshaa kupanda miti bilioni 1 ifikapo mwaka 2030 ili kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa nchini humo.
Komaza inajishughulisha na upandaji wa miti kibiashara kwa lengo la kuwanufaisha wakulima nchini humo na Kusini mwa Jangwa la Sahara kwa kuwapatia mazingira rafiki ya kilimo.
Fedha hizo zimetolewa na kampuni ya Novastar Ventures ambayo inasaidia kampuni zinazochipukia ikishirikiana na mameneja wa uwekezaji wa kampuni hiyo ili kuisaidia Komaza kuongeza vituo vya uzalishaji wa miti ili kukabiliana na athari za ukataji wa miti hasa inayotumika katika shughuli za ujenzi.
Zinazohusiana
- Kampeni ya mtandaoni inavyochagiza upandaji miti duniani
- Kutana na kijana aliyedhamiria kupanda miti milioni 20 ifikapo Januari 2020
Kwa kutumia fedha hizo, kampuni hiyo itashirikiana na wakulima kupanda miti hiyo katika maeneo yao kuhakikisha inawapatia mazingira rafiki kwa kilimo na kujipatia kipato kwa kuuza miti kwa wanunuzi.
Hadi sasa, Komaza imeshirikiana na wakulima zaidi ya 6,000 ambapo kwa kipindi chote tangu kuanzishwa kwake, imepanda miti milioni 2 huku ikitumia teknolojia ya “Artificial intelligency (AI)” kukusanya taarifa za miti iliyopo.
Latest
