Sifa za simu mpya za Samsung zilizoingia sokoni Agosti 7

August 19, 2019 1:54 pm · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Samsung imeingiza simu aina ya “Note 10” na “Note 10 plus”
  • Simu hizo ambazo ni matoleo mapya zinachuana kwa viwango vya ubora. 
  • Uwezo wa betri, ukubwa wa kioo na gharama ni baadhi ya sifa nzuri kwenye simu hizo. 

Dar es Salaam. Kampuni ya simu za mkononi na vifaa vya kielektroniki ya Samsung tayari imeingiza sokoni matoleo mapya  ya simu za “Samsung Note 10” na “Note 10 plus”, ikiwa ni hatua ya kuendeleza ushindani wa simu za kisasa duniani.  

Matoleo hayo ya simu yaliingia sokoni Agosti 7, 2019 lakini bado watumiaji wake wamekuwa na maswali ni simu ipi ambayo itakidhi mahitaji yao ya mawasiliano hasa wale ambao wanakwenda na wakati.

Nukta (www.nukta.co.tz)  inakuletea uchambuzi wa sifa za simu hizo mbili ambao utakupa urahisi wa kuchagua ni simu ipi itakufaa kulingana na ubora na unene wa mfuko wako. 

Gharama ya simu hizo mbili

Kwa wanunuzi wa Tanzania wanaweza kuzipata simu hizo kwa kuweka oda kupitia kampuni ya simu ya Tigo. Simu ya Note 10 inapatikana kwa takriban Sh2.5 milioni huku Note 10+ ikipatikana kwa sh2.9 milioni. 

Ukubwa wa kioo

Note 10+ ina ukubwa wa inchi 6.8 kwenye kioo chake huku kioo cha Note 10 kioo kikiwa na ukubwa wa inch 6.3, jambo linalofanya kioo cha note 10+ kuwa kikubwa kuliko simu zyeyote aina ya “Note” iliyowahi kutokea. 

Ukubwa huo umefanya simu ya Note 10+ kuwa simu bora kwa wapenzi wa michezo ya kielektroniki “Games” na hata wahariri wa video pamoja na wanasanaa.

Muonekano wa Note 10. Picha| Mtandao.


Zinazohusiana


Muonekano wa kioo (Display)

Simu zote zinatumia muundo wa screen ya kisasa ya “Gorilla glass 6” ambazo pia zinatumika kwenye simu kama OnePlus 6T, Samsung Galaxy S10+, Xiaomi Mi 9 na Sony Xperia 1. 

Hata hivyo, bado Note 10+  imeizidi “pixel” kadhaa Note 10 yenye pixel 1020×2280 kwani Note 10 plus ina pixel 1440×3040 hivyo kuifanya watumiaji wanao zingatia “pixel” kuchagua simu hii dhidi ya Note 10.

Ubora wa kamera

Japo Samsung hawajatofautisha lenzi na “sensor” za simu hizi na zile za kwenye toleo la “S Series ya S10”, simu zote zina kamera tatu nyuma. Kati ya kamera hizo, kuna lensi ya “Ultra wide” yenye megapixel 16, lensi ya “wide angle” yenye megapixel 12 na lenzi ya “telephoto” yenye megapixel 12 yenye “optical zoom” mara mbili.Pamoja na hayo, simu hizo zina kamera ya mbele yenye megapixel 10 ambayo ni megapixel 3 tofauti na toleo la i phone x zenye megapixel 7.

Ukiachilia mbali Note 10 plus kuwa na “sensor” ya ziada inayowezesha kupiga picha aina ya “potrait” kama zile za Iphone kuanzia toleo la 7, kamera za simu hizi zinafanana kwani zote zina “Live focus mode” inayowezesha “kuangalia kitu au mtu wakati wa kuchukua video pamoja na maiki ya “zoom in” inayochuja sauti zisizotakiwa wakati wa kurekodi sauti.

Hivyo kufanya simu hii kuwa simu nzuri kwa wanahabari na hata wasanii wa muziki wanaotumia mfumo wa kurekodi mara kwa mara.

Ikiwa na inchi 6.8 kama ukubwa wa kioo chake, Note 10+ ni kubwa kuliko  simu aina ya “Note” zote Picha|Mtandao.

Uhifadhi kumbukumbu

Note 10 plus inajitofautisha na Note 10 kwenye sehemu tatu. Kati ya sehemu hizo ni uwezo wa kuhifadhi kumbukumbu ambapo Note 10 ina RAM ya GB12 huku Note 10 ikiwa na GB 8 tu. Hii ni sawa na kusema Note 10+ ina uwezo wa kufanya vitu vingi kwa wakati mmoja “Multitasking” kuliko Note10.

Hata hivyo, uwezo huo bado ni mkubwa ukilinganisha na ule wa iPhone XS Max na Pixel 3 XL ambazo zote zina ukubwa wa GB 4 tuu za RAM huku Note 9 ikiwa na GB9.

Kwa sasa bado “Note 10 na 10+” zinaongoza matoleo mengi kwani zina hifadhi kumbukumbu hadi kwa uwezo wa zaidi ya GB 250. Changamoto ya Samsung Note 10 hazina sehemu ya kuweka kadi ya kumbukumbu “memory card” jambo, wakati Samsung Note 10 plus inakupa hadi GB512 za  na nafasi ya kuweka kadi ya kumbukumbu hadi ukubwa wa “terabite” 1.

Uwezo wa Betri

Note 10 plus inabaki kuwa kileleni kuliko simu yoyote ya Samsung kwani betri yake ina uwezo wa 4,300mAh jambo inayoifanya idumu kwa muda wa zaidi ya saa 10 ikichajiwa vizuri huku betri la Note 10 likiwa na uwezo wa 3,500mAh tu.

Enable Notifications OK No thanks