Si kweli: Spika wa Gabon hajakamatwa akitoroka na hela baada ya mapinduzi

September 5, 2023 9:16 am · Daniel Mwingira
Share
Tweet
Copy Link
  • Video zinazosambaa zilichapishwa tangu mwaka 2022.
  • Ni Spika mstaafu wa Bunge la Gabon aliyekamatwa akiwa na zaidi ya faranga bilioni moja.

Dar es Salaam. Agosti 30, 2023 ulimwengu uliamka na taarifa ya mapinduzi ya kijeshi yaliyofanyika nchini Gabon, ambapo Jenerali Oblice Oligui Nguema alimpindua Rais mteule wa taifa hilo la Afrika ya Kati Ali Bongo aliyekaa madarakani kwa muda wa miaka 14.

Mara baada ya mapinduzi hayo kumekuwa na taarifa nyingi za uzushi ikiwemo ile ya Spika wa Bunge la Gabon kukamatwa akiwa na mabegi yaliyojaa fedha wakati akitoroka.

Taarifa hiyo ilichapishwa Agosti 31,kupitia mtandao wa X zamani ukijulikana kama Twitter  ambapo akaunti nyingine katika mtandao huo huo  mtandao huo wa X ulichapisha habari kama hiyo kuwa kuna kiongozi mwingine wa Serikali iliyopinduliwa amekamatwa na mabegi yenye fedha wakati akijaribu kutoroka.

Tulichokibaini

Nukta Fakti baada ya kufanya tafiti tumebaini  kuwa ni kweli moja video hizo ni za kweli ingawa haihusiani kabisa na mapinduzi yaliyotokea ambapo kupitia zana ya Google Reverse Search image tumebaini video hiyo imewahi kutumika mwaka 2022.

Mathalani video kama hiyo ilishawai kuchapisha kwenye chaneli  ya YouTube ya EDUSPLORER 21, September 2022 ikiwa na kichwa cha habari ‘Gabon: Opposition Leader Arrested With Suitcases Full of Banknotes Worth 77 Million Euros Guy Nzouba’ kikiwa na maana kiongozi wa upinzani amekamatwa akiwa na fedha zenye thamani ya Euro milioni 77.

Aidha, habari hiyo imeshawahi kuchapishwa Septemba 18, 2022, kupitia akaunti ya mtandao wa YouTube ya TV5 Monde ikiwa na maelezo katika lugha ya Kifaransa 

Kwa msaada wa Google translate tumebaini kuwa maelezo hayo hayahusiana na tukio la mapinduzi bala ni “Guy Nzouba-Ndama, aliyekuwa Rais wa Bunge la Taifa la Gabon, alikamatwa akiwa na zaidi ya faranga bilioni moja za Afrika ya Kati.

Vilevile, Nukta Fakti imebaini kuwa anayeonekana kwenye video hiyo anaitwa  Guy Nzouba-Ndama, ambaye ni Rais wa Zamani wa Bunge la Gaboni ambaye baadae alihamia chama pinzani.

Spika wa sasa wa Bunge la Gabon anaitwa Boukoubi Faustin ambaye ndiye alikuwa anaongoza Bunge hadi mapinduzi yanatokea.

Hivyo ni kweli Guy Nzouba -Ndama alikamatwa na fedha lakini sio kweli alikamatwa baada ya  mapinduzi yaliyotokea siku ya Agosti 30, 2023.

Enable Notifications OK No thanks