Shilingi ya Tanzania yaimarika dhidi ya Dola
- Viwango hivi vya kubadili fedha vinaendelea kuonyesha umuhimu wa kufuatilia mwenendo wa Shilingi dhidi ya sarafu kuu.
Dar es Salaam. Shilingi ya Tanzania imeendelea kuonyesha nguvu dhidi ya Dola ya Marekani, hali inayotoa taswira ya mwenendo wa sarafu hiyo katika soko la fedha nchini.
Kwa mujibu wa viwango vya kubadilisha fedha vya Leo Septemba 9, 2026, Benki ya CRDB inanunua Dola moja kwa Sh2,600 na kuuza kwa Sh2,680, wakati Benki ya NMB inanunua kwa Sh2,595 na kuuza kwa Sh2,675.
Hii ina maana kuwa mteja mwenye Dola moja, akiiuza benki anaweza kupata hadi Sh2,600 CRDB, huku anayehitaji kununua Dola moja kutoka benki hiyo atahitaji Sh2,680.
Kwa upande wa NMB, Dola moja inanunuliwa kwa Sh2,595 na kuuzwa kwa Sh2,675, hivyo tofauti ya viwango kati ya benki hizo mbili ni Sh5 kwa Dola katika bei ya kunununa kuuza.
Mwenendo huo una umuhimu kwa wafanyabiashara, wasafiri, waagizaji wa bidhaa kutoka nje na watu wanaofanya miamala ya kimataifa, kwa kuwa thamani ya Shilingi dhidi ya Dola huathiri moja kwa moja gharama za bidhaa na huduma zinazolipiwa kwa fedha za kigeni.
Sarafu nyingine
Mbali na Dola, viwango vya benki vinaonyesha kuwa Euro inanunuliwa kwa Sh2,924.25 na kuuzwa kwa Sh3,224.25 CRDB, huku Benki ya NMB ikiweka viwango vya Sh2,901 na Sh3,201 mtawalia.
Kwa sarafu za Afrika Mashariki, Shilingi ya Kenya inanunuliwa kwa Sh16.95 CRDB na Sh17.8 NMB, wakati Shilingi ya Uganda inanunuliwa kwa Sh0.675 na Kuuzwa Sh0.62.
Kwa ujumla, viwango hivi vinaendelea kuonyesha umuhimu wa kufuatilia mwenendo wa Shilingi dhidi ya sarafu kuu, hasa Dola ya Marekani, ambayo hutumika kwa kiasi kikubwa katika biashara ya kimataifa na malipo ya bidhaa zinazoagizwa kutoka nje ya nchi.
