Sh44.1 bilioni za Uswiss zitakavyonufaisha kaya masikini Tanzania

October 7, 2020 6:44 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Zitasaidia kuboresha huduma za afya na elimu.
  • Pia zitakuwa chachu ya kuimarisha nguvukazi ya watu kwenye kaya masikini. 
  • Serikali yasema itahakikisha fedha hizo zinatumika kama zilivyokusudiwa. 

Dar es Salaam. Watanzania hasa wale wanaoishi katika kaya masikini wana kila sababu ya kutabasamu kutokana na msaada wa Sh44.1 bilioni uliotolewa na nchi ya Uswiss ili kuboresha nguvukazi na huduma za jamii ikiwemo afya na elimu Tanzania. 

Msaada huo ni kwa ajili ya awamu ya pili ya mpango wa kunusuru kaya masikini chini ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (Tasaf) unaotekelezwa kwa kipindi cha miaka minne kuanzia mwaka 2020 hadi 2023 na kuchangia Mfuko wa Pamoja wa Afya kwa mwaka wa fedha 2020/21.

Mikataba wa misaada hiyo imesainiwa jijini Dodoma Oktoba 6, 2020 na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Doto James kwa niaba ya Serikali ya Tanzania na Balozi wa Uswiss nchini Tanzania, Didier Chassot kwa niaba ya Serikali ya Uswiss.

James, amesema kati ya fedha zilizotolewa, Sh39.15 bilioni ni kwa ajili ya Tasaf ambapo zitasaidia kuboresha maisha ya kaya masikini Tanzania. 

“Msaada kwa ajili ya Tasaf utasaidia kupunguza umasikini na kuboresha nguvukazi, kuboresha uwezo wa kununua mahitaji ya kaya masikini, kuongeza uandikishwaji wa watoto shuleni na kuimarisha huduma za jamii,” amesema James. 

Fedha zilizobaki ambazo zitaenda katika Mfuko wa Pamoja wa Afya zitasaidia kuboresha utendaji wa watoa huduma ya afya ya msingi, kuhakikisha huduma bora za afya zinatolewa na kuwezesha utekelezaji wa mpango mkakati wa sekta ya afya pamoja na malengo yake.

Mfuko wa Afya wa Pamoja ulioanzishwa mwaka 1999 na umefanikiwa kuboresha huduma za afya katika zaidi ya kaya 184 Tanzania. 


Soma zaidi: 


Balozi wa Uswiss nchini Tanzania, Didier Chassot amesema fedha hizo zilizotolewa zitasaidia kutunisha mfuko huo ili kuongeza wigo wa utoaji wa huduma za afya nchini.

“Kusainiwa kwa makubaliano ya msaada wa leo kutaruhusu kuendelea kuchangia mpango wa afya kwa wote nchini na tutaendelea kuwekeza katika mfuko huu”, amesema Balozi Chassot.

Amesema wakati Tanzania inapiga hatua kiuchumi ni lazima pia kulinda maisha ya watu ambao hawajanufaika kikamilifu na ukuaji huo wa uchumi.

Mpango wa pili wa Tasaf ulioanza mwaka 2020/2021 umepanga kutumia Sh2.02 trilioni kuzifikia kaya masikini katika vijiji na mitaa ambayo haikufikiwa wakati wa kutekeleza mpango wa Tasaf awamu ya kwanza.

Kwa mujibu wa Wizara ya Fedha na Mipango, mpango wa Tasaf awamu ya kwanza ulitekelezwa mwaka 2013 hadi mwaka 2019 ambapo kaya milioni 1.1 zenye watu milioni 5.3 katika Serikali za Mitaa 159 Tanzania Bara na Zanzibar, zilinufaika na ufadhili huo.

Pia hatua hiyo imewezesha watoto milioni 1.8 kuandikishwa elimu ya msingi na  wanafunzi 448,409 wamesomeshwa elimu ya sekondari katika kaya 1.1 zilizonufaika. 

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jul, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
16 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
16 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Kutana na ‘Poultry Plucker’, mashine inayonyonyoa kuku watatu kwa dakika moja

Kutana na ‘Poultry Plucker’, mashine inayonyonyoa kuku watatu kwa dakika moja

Nukta TV

Rais Samia: Kalamu yangu ina hatari, sijawahi kusaini mtu kunyongwa

Rais Samia: Kalamu yangu ina hatari, sijawahi kusaini mtu kunyongwa

Nukta TV

Rais Samia: Matumizi jina Samia, likiwa kila mahali inachosha, tafuteni wengine

Rais Samia: Matumizi jina Samia, likiwa kila mahali inachosha, tafuteni wengine

Nukta TV