Sh42 bilioni zatumika kukarabati nusu ya shule kongwe za sekondari

February 25, 2019 9:36 pm · Nuzulack Dausen
Share
Tweet
Copy Link
  • Fedha hizo zitatumika kukarabati shule hizo kongwe kati ya 88 zilizopo nchini ikiwemo Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Ruvu iliyopo mkoani Pwani.
  • Miongoni mwa changomoto kubwa ambazo shule nyingi za umma zinakumbana nazo ni ufinyu wa bajeti unaofanya washindwe kumudu utoaji wa elimu bora.

Dar es Salaam. Serikali imeeleza kuwa imetoa zaidi ya Sh42 bilioni kutekeleza mradi wa kukarabati miundombinu ya shule kongwe za sekondari 42 katika jitihada za kurudisha hadhi shule hizo ambazo zilitamba kitaaluma miaka ya nyuma.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Wizara ya Fedha na Mipango leo (Februari 25, 2019) inaeleza kuwa fedha hizo zitatumika kukarabati shule hizo kongwe kati ya 88 zilizopo nchini ikiwemo Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Ruvu iliyopo mkoani Pwani.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dk Ashatu Kijaji amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha kuwa shule zote kongwe, zenye historia kubwa ya kutoa viongozi wengi na wataalam mbalimbali nchini, zinakuwa na hadhi na kuwa kimbilio la wananchi.

Mapema Agosti mwaka jana Serikali ilieleza kuwa zaidi ya Sh200 bilioni zitatumika katika mchakato wa kukarabati shule hizo kongwe nchini ambazo sehemu kubwa zimeshapotea katika orodha ya shule 10 bora. 

“Dhamira yetu ni kuona watoto wetu wanasoma kwenye mazingira sahihi na ufaulu wao unaongezeka kwa sababu tunawaandaa wataalam wa kesho wa Taifa letu,” amesema Dk Kijaji.


Soma zaidi: 


Kiongozi huyo ameutaka uongozi wa Sekondari ya Wasichana Ruvu kuhakikisha wanatoa elimu bora ili thamani ya uwekezaji mkubwa wa Serikali unaofikia zaidi ya  990 milioni uweze kuonekana. 

Taarifa hiyo ya wizara iliyotolewa na Msemaji wake, Ben Mwaipaja inaeleza kuwa Dk Kijaji amejionea ukarabati uliofanyika shuleni hapo na kwamba bado nyumba sita za walimu hazijakarabatiwa pamoja na kutonunuliwa kwa samani za shule vikiwemo vitanda.

Dk Kijaji ameahidi kuifanyia kazi changamoto hiyo wakati huu wa mchakato wa bajeti mpya. Serikali kwa sasa ipo katika mchakato wa kuandaa bajeti mpya ya mwaka wa fedha 2019/2020. 

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dk Ashatu Kijaji (wa pili kushoto) akitoa maelekezo kwa viongozi wa Shule Kongwe ya Sekondari ya Wasichana Ruvu Mkoani Pwani, kuhakikisha maboresho ya shule hiyo yanakwenda sambamba na ufanisi katika utoaji taaluma, wakati alipofanya ziara shuleni hapo. Kulia ni Mbunge wa Kibaha Vijijini, Hamoud Juma na kushoto ni Mkuu wa Shule  hiyo, Juliana Chimazi.

Mwishoni mwa wiki iliyopita Dk Kijaji alisitisha ukaguzi wa Shule ya Sekondari ya Pugu Jijini Dar es Salaam baada ya viongozi wa Manispaa ya Ilala kushindwa kueleza mradi kwa kina. 

Miongoni mwa changomoto kubwa ambazo shule nyingi za umma zinakumbana nazo ni ufinyu wa bajeti unaofanya washindwe kumudu utoaji wa elimu bora kutokana na uhaba wa walimu, vifaa vya kufundishia na miundombinu muhimu yakiwemo madarasa na maabara. 

Mkuu wa shule hiyo Juliana Chimazi amesema shule hiyo inahitaji vitanda vipya kwa kuwa vilivyopo vimedumu zaidi ya miaka 50 pamoja na kuomba fedha kwa ajili ya kukamilisha ukarabati wa nyumba sita za walimu.

Miongoni mwa miundombinu iliyoboreshwa katika shule hiyo ni pamoja na mifumo ya maji taka, madarasa, vyoo, mabweni, nyumba za walimu na ofisi.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
17 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
17 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
17 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Siku ya Familia, Mtoto wa Afrika kuadhimishwa Juni 30, 2026

Siku ya Familia, Mtoto wa Afrika kuadhimishwa Juni 30, 2026

Nukta TV

Wadau wa 'kubet" watoa ya moyoni, pendekezo kupanda kwa tozo 5%

Wadau wa 'kubet" watoa ya moyoni, pendekezo kupanda kwa tozo 5%

Nukta TV

Wasemayo wananchi, vocha za kukwangua kupigwa maruku mijini

Wasemayo wananchi, vocha za kukwangua kupigwa maruku mijini

Nukta TV