Serikali yamwaga ajira zaidi ya 21,000 za watumishi wa afya, elimu

April 12, 2023 12:04 pm · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Rais Samia ameridhia kibali cha kuajiri watumishi 21,200 wa kada za ualimu na afya, jambo likalosaidia kupunguza uhaba wa watumishi katika sekta hizo nyeti nchini.

Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan ameridhia kibali cha kuajiri watumishi 21,200 wa kada za ualimu na afya, jambo likalosaidia kupunguza uhaba wa watumishi katika sekta hizo nyeti nchini. 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Angellah Kairuki katika taarifa yake iliyotolewa leo Aprili 12, 2023 amesema kati ya watumishi hao, 13,130 ni walimu wa sekondari na msingi na waliobaki ni watumishi wa afya watakaofanya kazi katika hospitali za halmashauri, vituo vya afya na zahanati.

Enable Notifications OK No thanks