Serikali ya Uganda haijatangaza fidia kwa majeruhi wa ajali iliyosababishwa na msafara wa Rais
- Hakuna taarifa rasmi kutoka ikulu ya Uganda inayoonyesha kuwalipa fidia majeruhi wa ajali.
- Serikali ya nchi hiyo kupitia ukurasa wa Twitter imewataka wananchi kupuuzia taarifa hiyo.
Dar es Salaam. Kama wewe ni mtumiaji wa mtandao wa Twitter hapana shaka umekutana na ujumbe unaosambaa kwenye mtandao huo unaodaiwa kutoka Ikulu ya Uganda ukiahidi kutoa fidia kwa majeruhi wa ajali iliyosababishwa na msafara wa Rais Yoweri Museveni Septemba 12, 2022. Ujumbe huo sio wa kweli.
Ujumbe huo uliosambazwa kupitia akaunti ya Twitter inayofanana na ile ya Ikulu ya Uganda umebeba maneno ya Kiingereza yanayosomeka:
“Tutatoa fidia kwa waathirika wa ajali waliofariki lakini tunawaonya watumiaji wa barabara kujifunza kuheshimu msafara wa Rais, tutawagonga na kuwaacha barabarani ikiwa mnafikiri mna umuhimu kuliko maisha ya Rais.”
Kupitia ukurasa rasmi wa Twitter wa Ikulu ya Uganda taarifa hiyo imewekewa alama nyekundu ikimaanisha ni habari ya uzushi na wamewataka wananchi kupuuzia ujumbe huo.
Tuliyobaini zaidi
Uchunguzi uliofanywa na timu ya NuktaFakti (www.nukta.co.tz) umebaini kuwa ukurasa rasmi wa Twitter wa Ikulu ya Uganda hauwajahi kuchapisha taarifa zozote kuhusu ajali au tamko lolote la kuwalipa fidia majeruhi wa ajali hiyo.
Neno “Tweet” kwenye kila ujumbe wa mtandao huu hukaa juu ya jina la akaunti (kama inavyoonekana hapo chini) na sio katikati kama inavyoonekana kwenye ujumbe huo wa uzushi unaosambaa.
Aina ya maandishi (font) iliyotumika kwenye ujumbe wa uzushi haifanani na aina za kawaida zinazotumika kwenye mtandao wa Twitter.
Pia matumizi ya lugha isiyo rasmi yaliyotumika kwenye ujumbe huo wa uzushi yanaashiria mwandishi siyo mtu aliyebobea kwenye mawasiliano ya taasisi kubwa kama Ikulu hivyo ujumbe huo wa uzushi si wa kweli.
Uamuzi wetu
Kupitia ushahidi ulioonekana hapo juu, ujumbe huu wa uzushi si wa kweli kuna uwezekano ukawa umetengenezwa kwa kutumia program hariri zenye uwezo wa kufuta na kuchapisha ujumbe mpya kwa kuiga ujumbe halisi akaunti husika.
Latest
![](https://i0.wp.com/nukta.co.tz/wp-content/uploads/2025/02/gold-loan2.jpg?fit=300%2C169&ssl=1)
![](https://i0.wp.com/nukta.co.tz/wp-content/uploads/2025/02/Broccoli_FP_img_0051.jpg?fit=300%2C200&ssl=1)
![](https://i0.wp.com/nukta.co.tz/wp-content/uploads/2025/02/2b03433c79fa3de3acb7dc5ba864ebd2.jpeg?fit=300%2C169&ssl=1)
![](https://i0.wp.com/nukta.co.tz/wp-content/uploads/2025/02/gold-loan2.jpg?fit=300%2C169&ssl=1)