Safari ya Yas Business kukuza matumizi ya IoT Tanzania

June 10, 2026 8:19 am · Kelvin Makwinya
Share
Tweet
Copy Link
  • IoT ni huduma ya kidijitali inayounganisha vifaa vya kielektroniki kupitia intaneti na kuviwezesha kuwasiliana, kukusanya taarifa na kuchukua hatua kwa papo hapo.

Dar es Salaam. Fikiria wewe ni mkulima, ukiwa safarini unaamka asubuhi na kukutana na ujumbe kwenye simu yako unaokueleza kuwa unyevu katika sehemu moja ya shamba lako umeshuka chini ya kiwango hitajika.

Bila ya kufika shambani, kupitia simu yako ya mkononi na intaneti imara, unaamuru mfumo wa umwagiliaji kuanza kumwagilia sehemu husika ili kuokoa mazao yaliyopo.

Hii si hadithi ya kufikirika au ‘movie’ bali ni maisha halisi ambayo Mtanzania wa sasa anaweza kuyaishi baada ya Yas Tanzania kuzindua huduma ya ‘Internet of Things (IoT)’ kama moja ya huduma zinazotolewa na Yas Business.

IoT au mtandao vitu ni huduma ya kidijitali inayounganisha vifaa vya kielektroniki kupitia intaneti na kuviwezesha kuwasiliana, kukusanya taarifa na kuchukua hatua kwa papo hapo (Real-time).

Kwa lugha rahisi, ni teknolojia inayofanya mashine, vifaa na mifumo mbalimbali kuoana, kusikia na kuwasiliana bila kusubiri binadamu afanye kila kitu mwenyewe jambo linalotoa muda zaidi kufanya shughuli nyingine za kiuzalishaji.

Msaidizi wa kweli

Josepher Muru, mmoja ya wataalamu waliokuwa wakionyesha teknolojia hiyo kwenye moja ya mabanda ya maonyesho wakati wa uzinduzi wa Yas Business, anasema wafanyabiashara na kampuni sasa wanaweza kutumia huduma hiyo kutokana na shughuli zao.

“Unaweza kuunganisha vifaa kama vile mfumo wa umwagiliaji, vifaa vya uchimbaji, mitambo ya viwandani au hata vifaa vya matumizi ya kawaida kama vile gari na kadhalika,” anasema Muru.

Ikiwa kiwanda kitaunganisha vifaa vya uzalishaji na IoT, anasema, kitapata taarifa zote ikiwemo hitilafu za kiufundi jambo linalopunguza hasara zitokanazo na kusimama kwa uzalishaji ambapo matatizo hujulikana baada ya vifaa kuzima.

Anasema katika sekta ya madini mchimbaji anaweza kuunganisha roboti ambalo anaweza kuliongoza kufanya shughuli zote za uchimbaji hususan katika sehemu ambazo binadamu wa kawaida hawezi kufika.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Yas Tanzania, Pierre Canton-Bacara anasema katika kuhakikisha kuwa wafanyabiashara wanaongeza tija, Yas imewekeza katika kuboresha upatikanaji wa mtandao wa intaneti.  Picha | Yas Tanzania.

Tanzania ni miongoni mwa nchi barani Afrika zenye rasilimali kubwa za madini zikiwemo dhahabu, almasi na Tanzanite huku kampuni kubwa, za kati na wachimbaji wadogo wadogo wakihusika zaidi katika uchimbaji. 

Hata hivyo, usalama huwa ni mdogo katika migodi ya wachimbaji wa kati na wadogo wasiofuata miongozo ya kiusalama migodini. Matumizi ya IoT yanaweza kupunguza kwa kiwango kikubwa cha hatari za kiusalama iwapo itatumika ipasavyo na kuunganishwa na intaneti yenye kasi na ubora wa juu. 

Afisa Mtendaji Mkuu wa Yas Tanzania, Pierre Canton-Bacara anasema katika kuhakikisha kuwa wafanyabiashara wanaongeza tija, Yas imewekeza katika kuboresha upatikanaji wa mtandao wa intaneti.  

Aliwaambia washiriki wa uzinduzi wa Yas Business kuwa kupitia teknolojia ya SD-WAN inayotolewa na kampuni hiyo, kampuni zinapata intaneti ya uhakika na yenye kasi ya hadi 5G bila kusuasua. 

SD- WAN kuongeza ufanisi wa mtandao

SD-Wan ama “Software-Defined Wide Area Network” kwa kimombo ni mfumo wa mtandao unaotumia programu ya kompyuta kusimamia na kuelekeza data kwa ustadi katika mtandao wa kampuni au shirika ili kuongeza upatikanaji wa intaneti. 

Moja ya faida ya teknolojia ya SD-WAN ni uhakika wa upatikanaji wa intaneti kwa kuwa humuamisha mtumiaji kwenye mtandao imara pale inapogundua ule wa awali umezidiwa zaidi na watumiaji. 

Yas Tanzania, iliyonunuliwa na Axian Telecom, miaka takriban minne iliyopita, imewekeza zaidi ya Sh1 trilioni kwenye upanuzi na uboreshaji wa mtandao nchi nzima. 

Kupitia teknolojia ya SD-WAN inayotolewa na kampuni ya Yas, kampuni zinapata intaneti ya uhakika na yenye kasi ya hadi 5G bila kusuasua. Picha | Yas Tanzania.

Emmanuel Mallya, Ofisa Mkuu wa Kitengo cha Teknolojia na Ufundi wa Yas anasema katika uboreshaji huo muhimu wameongeza zaidi ya minara 1,600 mijini na vijijjini ambapo kiwango cha chini ni mtandao wa 4G. 

Mallya anasema kuhakikisha kampuni na wafanyabiashara wanapata intaneti ya kasi ambayo inahitajika zaidi katika matumizi ya IoT, Yas inaweza kumjengea mnara maalum au mnara mdogo mfanyabiashara husika ili kuimarisha ufanisi katika uzalishaji.  

“Tuna zaidi ya minara 600 ya 5G mijini na kwenye majiji…tuna mtandao mpana wa 4G na 5G nchini nzima, unaweza kufanya kazi popote pale,” alieleza Mallya katika uzinduzi huo uliohudhuriwa na vigogo na wadau mbalimbali wa mawasiliano na teknolojia. 

Suluhu hitajika kibiashara

Kwa muda mrefu, miradi na kampuni nyingi zimekuwa zikikabiliwa na changamoto ya ukosefu au udhaifu wa intaneti unaosababishwa na umbali au eneo ambalo mradi husika unatekelezwa. 

Udhaifu wa intaneti ni miongoni mwa vizingiti vilivyokuwa vikipunguza kasi ya matumizi ya teknolojia ya IoT katika shughuli mbalimbali za kiuzalishaji nchini. 

Mkakati wa Uchumi wa Kidijitali 2024 – 2034 wa Tanzania unaeleza kuwa IoT inaweza kuchangia katika maendeleo ya miji ya kisasa ambapo vifaa na vihisi au ving’amuzi (sensors) vilivyounganishwa vinaweza kuboresha miundombinu ya mijini, ikiwa ni pamoja na usimamizi wa trafiki, usimamizi wa taka, nishati endelevu, miundombinu ya kidijitali, na usambazaji wa nishati. 

Yas Business itaweza kuondoa vikwazo katika ufanyaji biashara Tanzania ikiwemo ukosefu wa ufanisi na gharama kubwa za uendeshaji biashara. Picha | Yas Tanzania.

Mkakati huo unaeleza miongoni mwa mifano ya matumizi ya IoT ni mradi ujao wa Mji wa Kisasa wa Bagamoyo (Bagamoyo Smart City), ukuaji wa vifaa vilivyounganishwa na faida zake kwa kaya za Kitanzania (nyumba za kisasa) zenye mifumo ya taa za kisasa pamoja na ulinzi na usimamizi wa hali ya juu.

‘Yas Business kuondoa vikwazo’

Pierre, bosi wa Yas, anasema Yas Business imeanzishwa kuondoa vikwazo katika ufanyaji biashara Tanzania ikiwemo ukosefu wa ufanisi na gharama kubwa za uendeshaji biashara. 

“Huduma muhimu kama hizi zinapaswa kuwa nafuu, unafuu ni muhimu sana,” anasema Pierre akibainisha kuwa Yas Business ni itasaidia katika ukuaji wa sekta mbalimbali zikiwemo za benki, uchukuzi, na viwandani. 

Uboreshaji wa upatikanaji wa intaneti yenye kasi isiyoyumba ni miongoni mwa hatua muhimu wa kuimarisha safari ya kuongeza matumizi ya IoT nchini Tanzania hususan katika kipindi cha uchumi wa kidijitali. 

Tanzania inalenga kuongeza uchumi wake kwa zaidi ya mara 10 kufikia uchumi wa Dola za Marekani trilioni 1 zaidi ya Sh2,627 trilioni ifikapo 2050 huku teknolojia kidijitali ikiwemo IoT ikitarajiwa kuchangia kwa kiwango kikubwa safari hiyo ya kiuchumi. Kwa sasa uchumi wa Tanzania ni Dola za Marekani bilioni 95 sawa na Sh249.6 trillion. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

/
No matches found for this filter
10 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
10 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
10 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mikakati ya Serikali kuhakikisha walimu wa VETA wanapata ajira na mikopo

Mikakati ya Serikali kuhakikisha walimu wa VETA wanapata ajira na mikopo

Nukta TV

Mama Salama alivyombana Wanu kuhusu maslahi ya walimu wanaojitolea

Mama Salama alivyombana Wanu kuhusu maslahi ya walimu wanaojitolea

Nukta TV

Kwanini uchafuzi wa mazingira ni tishio kwa afya ya binadamu na uchumi

Kwanini uchafuzi wa mazingira ni tishio kwa afya ya binadamu na uchumi

Nukta TV