Rushwa yapungua Tanzania – Transparency International

July 12, 2019 8:26 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Rushwa katika upatikanaji wa vitambulisho yaongezeka.
  • Rushwa katika ofisi ya Rais, Waziri Mkuu, viongozi wa kimila yashuka kwa kasi.
  • Zaidi ya nusu au asilimia 55 ya Waafrika wanaona rushwa imeongezeka katika nchi zao.

Dar es Salaam. Ripoti mpya ya Shirika la Kimataifa la Transparency International imebainisha kuwa kiwango cha rushwa Tanzania kimeshuka huku rushwa katika ofisi ya Rais, viongozi wa dini, wabunge na viongozi wa kimila ikipomoroka kwa kasi.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo iitwayo ‘Global Bribery Barometer-Africa 2019: Citizens’ views and esperiences of corruption” iliyozinduliwa jana (11 Julai 2019) nchini Ujerumani, kiwango cha rushwa Tanzania kimeshuka kutoka asilimia 25 mwaka 2015 hadi asilimia 18 mwaka 2019.

Ripoti hiyo inaeleza kuwa takriban robo tatu ama asilimia 72 ya waliohojiwa katika utafiti huo nchini walieleza kuwa kiwango cha rushwa kimeshuka huku asilimia 13 au mmoja kati ya watu 10 akieleza kuwa kimeongezeka ndani ya kipindi cha miezi 12 iliyopita.

Maeneo ya huduma za jamii za umma ambayo kiwango cha rushwa kimeshuka ni pamoja na shule kutoka asilimia 11 mwaka 2015 hadi asilimia nne mwaka huu.

Mengine ni kliniki na vituo vya afya vya umma ambapo kiwango cha rushwa kimeshuka hadi asilimia 11 mwaka 2019 kutoka asilimia 20 mwaka 2015.


Soma zaidi: 


Hata wakati rushwa katika huduma za umma ikishuka, Watanzania wengi wameeleza katika ripoti hiyo kuwa rushwa katika upatikanaji wa vitambulisho imepaa hadi asilimia 20 mwaka huu kutoka asilimia 15 mwaka 2015.

Hii ina maana kuwa kwa sasa watu 20 kati ya 100 nchini wanaona kuna kiwango kikubwa cha rushwa katika upatikanaji wa vitambulisho ukilinganisha 15 kati ya 100 waliokuwa na mtazamo huo mwaka 2015.

Katika ngazi ya taasisi, ofisi ya Rais, viongozi wa kimila, viongozi wa kidini na bunge ni miongoni mwa taasisi zilizopiga hatua kubwa zaidi katika kupunguza viwango vya rushwa katika kipindi hicho cha miaka minne.

Ripoti hiyo inabainisha kuwa mtazamo wa wananchi juu ya uwepo wa rushwa katika Ofisi ya Rais na Waziri Mkuu umeshuka zaidi ya mara tatu kutoka asilimia 15 mwaka 2015 hadi asilimia 4 mwaka huu.

Kwa sasa ni watu wanne tu kati ya 100 wanadhani ofisi hiyo ina rushwa ikilinganishwa na watu 15 kati ya 100 waliokuwepo mwaka 2015.

Maeneo ya huduma za jamii za umma ambayo kiwango cha rushwa kimeshuka ni pamoja na shule kutoka asilimia 11 mwaka 2015 hadi asilimia nne mwaka huu. Picha|Mtandao.

Mbali na ofisi hiyo, utafiti huo unaeleza kuwa mtazamo wa watu kuwa wabunge ni wala rushwa umeshuka mara tatu kutoka asilimia 21 mwaka 2015 hadi asilimia 8 mwaka huu.

Licha ya mafanikio hayo, bado rushwa miongoni mwa vigogo katika sekta ya biashara imeongezeka kidogo.

Ripoti hiyo inabainisha kuwa kiwango cha watu wenye mtazamo kuwa viongozi wa biashara ni wala rushwa kimepanda kwa asilimia moja kutoka asilimia 31 mwaka 2015 hadi asilimia 32 mwaka huu.

Utafiti huo ulichunguza mitizamo ya watu juu ya hali ya rushwa katika nchi 35 barani Afrika ikiwemo Tanzania. Matokeo ya jumla barani Afrika yanaonyesha kuwa zaidi ya nusu au asilimia 55 ya Waafrika wanaona rushwa imeongezeka katika nchi zao.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwenendo wa deni la serikali

Mwenendo wa deni la serikali

Nukta TV

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Nukta TV

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Nukta TV