Tamisemi yaomba Sh9.14 trilioni

April 14, 2023 8:39 am · admin
Share
Tweet
Copy Link
  • Fedha hizo ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na miradi ya maendeleo mwaka 2023/24. 
  • Asilimia 38.1 ya bajeti hiyo kuelekezwa katika miradi ya maendeleo. 

Dar es Salaam. Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) imeliomba Bunge liidhinishe Sh9.1 trilioni kwa matumizi ya kawaida na miradi ya maendeleo kwa mwaka 2023/24 ikiwa ni ongezeko la Sh366 bilioni kutoka bajeti iliyoombwa ya mwaka jana. 

Waziri wa Tamisemi Angellah Kairuki aliyekuwa akisoma hotuba ya makadirio na mapato ya wizara hiyo kwa mwaka 2023/24  leo Aprili 14, 2023 amewaambia wabunge kuwa kati ya fedha hizo Sh5.6  ni kwa ajili ya shughuli za kawaida huku Sh3.48 trilioni ni kwa ajili matumizi ya maendeleo.

Sasa naomba Bunge lako Tukufu likubali kuidhinisha Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2023/24 jumla ya Sh9.144 trilioni kati ya fedha hizo Sh5.65 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida yanayojumuisha mishahara ya walimu.

“Sh3.48 trilioni kwa ajili ya shughuli za maendeleo na Sh 1.06 kwa trilioni kwa ajili ya matumizi mengineyo,” amesema Kairuki bungeni jijini Dodoma.

Enable Notifications OK No thanks