Maumivu: Bei za mafuta zapaa

March 8, 2018 6:07 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Watumiaji kutoka mikoa ya Kaskazini mwa nchi wao hawataguswa na maumivu ya bei mpya za mafuta kwa kuwa Bandari ya Tanga haikuingiza shehena mpya ya nishati hiyo.

Dar es Salaam. Watumiaji wa mafuta nchini watalazimika kutoboa mifuko yao zaidi baada ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) kutangaza bei mpya za rejareja za nishati hiyo ambazo mwezi huu zimepaa ikilinganishwa na Februari kutokana na mabadiliko katika soko la dunia, kuongezeka kwa gharama za usafirishaji wa mafuta na kushuka kwa thamani ya Shilingi dhidi ya Dola ya Marekani.

Hata hivyo, maumivu hayo hayatawagusa wakazi wa mikoa ya Kaskazini kwa kuwa bei za mafuta hazijabadilika kwa kuwa Bandari ya Tanga haikuingiza mzigo mpya mwezi uliopita.

Katika bei hizo mpya, Ewura inaeleza kuwa watumiaji wa Dizeli watalipa Sh69 zaidi kwa lita ikilinganishwa na ilivyokuwa Februari wakati wale wa Petroli watatakiwa kuongeza Sh1 kwa lita. Watumiaji wa Mafuta ya Taa wao watalipa Sh4 kwa lita zaidi ya ilivyokuwa Februari. 


Soma zaidi: Shule 24 vigogo ‘zilizoteka’ 10 bora kidato cha nne


“Ifahamike kwamba katika shehena sita za mafuta zilizopokelewa katika Bandari ya Dar es Salaam katika mwezi Februari, tano zilinunuliwa kwa bei ya soko la dunia za Disemba 2017 na moja ilinunuliwa kwa bei ya soko la dunia ya mwezi Januari 2018,” inasomeka sehemu ya taarifa ya Ewura iliyotolewa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Nzinyangwa Mchany. 

Enable Notifications OK No thanks