Kinga ni bora kuliko tiba: Serikali ya Tanzania yaongeza kasi chanjo ya Corona

Herimina Mkude 0833Hrs   Septemba 28, 2021 Chati & Data
  • Idadi ya vituo vya kutolea chanjo ya Uviko-19 yaongezwa.
  • Ikiwa ni hatua ya serikali katika kurahisisha upatikanaji wa chanjo hiyo.

Dar es Salaam. Serikali ya Tanzania imeongeza juhudi katika kuongeza ushiriki wa wananchi katika kuchanja chanjo ya Uviko-19, ikiwa ni moja ya hatua za kuongeza idadi ya watu kuchanjwa ili kupambana na janga la Corona nchini. 

Tangu kampeni ya kutoa chanjo ya Uviko-19 ianze mwanzoni mwa Agosti 2021, dozi 400,000 zimetolewa hadi Septemba 26 kati ya zaidi ya milioni aina ya Johnson & Johnson zilizoingizwa nchini kupitiz mpango wa Covax. Kiwango hicho ni asilimia 38 ya dozi zote za chanjo zilizopokelewa Tanzania. 

Katika kuongeza hamasa ya watu kujitokeza kuchanja, Tanzania imeongeza juhudi za kuwafikia watu wengi zaidi ikiwa ni pamoja na kuongeza idadi ya vituo vya kutolea chanjo hiyo kutoka vituo 550 hadi vituo 6,784 ili kurahisisha upatikanaji wa huduma hiyo.Vilevile, Serikali imeongeza uhamasishaji na utoaji elimu kwa wananchi kuhusu chanjo ya Uviko-19 kupitia kampeni ya nyumba kwa nyumba.

Katika hatua nyingine, Serikali ya Tanzania inakamilisha taratibu za kuleta chanjo nyingine aina ya ‘Sinopharm’ dozi milioni 2 kutoka nchini China, idadi itakayofanya jumla ya chanjo zilizopokelewa kufikia milioni 3.

Related Post