Filamu ya kuchangamsha sikukuu za mwisho wa mwaka

December 24, 2021 12:53 pm · Herimina
Share
Tweet
Copy Link
  • Filamu hii ya “A Naija Christmas”, inahusu vijana watatu wenye msimamo wa kutokuoa.
  • Mama yao anaamua kuweka dau la nyumba ili kuwashawishi.vijana hao kubadilisha msimamo wao.

Dar es Salaam. Kama hujapata mualiko wa Christmas najua utakuwa umeshika tama ukiwaza siku kuu yako itaendaje, na kama huna “kahela” ka kujitoa “out” kwenda kusafisha macho ndiyo kabisa unaweza ukahisi umeachwa peke yako dunia nzima.

Lakini “Santa” wako yupo hapa kukutolea upweke kwa kukuletea filamu ambayo itakuchangamsha na kukufanya ufurahie siku kuu yako kitofauti kabisa. 

Ni filamu ya “A Naija Christmas”, iliyotengenezwa katika mazingira ya familia za kiafrika kabisa na katika namna ya kusherehekea Christmas.

Filamu hii inahusu familia ya Madam Agatha, singo mama mwenye vijana wa kiume watatu Chike, Obi, na Ugo.

Mama huyu ni wa makamo na licha ya kuwa ni “don” anaishi kwa mawazo kutokana na vijana wake kutokuwa na mpango wakuoa wala kumletea wajukuu.

Kwa mazingira ya kiafrika unaweza ukavuta picha vile wazazi huchanganyikiwa wakiona watoto wao umri ukienda lakini hawafikiri kuanzisha familia. 

Utaona wakihuzunika kila wakati na pengine kujiuliza kwanini waliwaleta duniani.

Kwa Madam Agatha anaamua asiendelee kujipa presha, hasa akikumbuka ya kuwa ameshafanya kila awezalo kuwashawishi vijana wake bila mafanikio.

Kwa awamu anaamua kucheza na akili za vijana wake. Anajua hakuna mtu anayeweza kukataa mali hivyo anaweka dau mezani. 

Dau hilo litakwenda kwa mwanaye anatakayekuwa wa kwanza kumletea mkwe wa halali nyumbani kwake. 

Ninavyosema wa halali, simaanishi mtu akajibebee tu binti wa watu huko aje naye, namaanisha binti aletwe akiwa ashavishwa pete na ndoa imefungwa kanisani.

Unajua ni dau gani kaweka? Mama huyu ameweka mezani hekalu  lake lenye kila samani.

Krismasi inapofika swali linabaki ni yupi kati ya vijana hawa atachukua mjengo?. Picha| Netflix

Kazi inabaki kwa watoto wake yaani, Chike, Obi na Ugo ambao wanatazamana kimshangao wakiwa hawaamini mama yao anachosema.

Msimamo wao ni kuwa hawana mpango wa kuoa lakini baada ya dau hilo, Je, wataendelea kushikilia misingi yao tena kwa uwepo wa dau nono kiasi hicho?

Hakuna mkate mgumu mbele ya chai

Ni vigumu kwa mtoto mwenye njaa kutokula kwa jirani kisa nyumbani amekatazwa na kwa mantiki hii vijana hawa msimamo wao unagonga mwamba.

Baada tu ya kupewa ahadi na mama yao, kila mtu anakimbilia chumbani kwake na kuanza kupigia “girlfriends” wake kuona kama katika wengi alokuwa nao walau anaweza ambulia mmoja wa kuoa.

Obi ambaye hajawahi kumtoa “out” hata “girlfriend” wake mmoja, siku hiyo anakuwa kama “customer care” kubembeleza apate “kadinner” na mmoja wapo.

Hakika madama Agatha awamu hii aliwaweza watoto wake maana harakati zinakuwa nyingi huku “stress” zikiamia kwao kutafuta wanawake ambao watamridhisha mama yao.

Kwa kiburi, madam Agatha anawafanya vijana wake wahahe kwani kila wanawake wanaowaleta anawakataa, huku akiwatishia kuahirisha ahadi yake endapo watazidi kuchelewa.

Vijana wanazidi kuchangayikiwa. Na kati yao, hakuna ambaye hataki kuondoka na hati ya mjengo.

Wanatoa ahadi kwa mama yao ambayo ni, “siku ya Christmas utasherehekea na wakwe zako”.

Bila shaka una shauku ya kujua ni nani aliyefanikiwa kumridhisha mama yake katika siku hiyo, au ni nani atakuwa wa kwanza kuoa na kukabidhiwa mjengo huo?

Basi, filamu ya “A Nija Christmas” ambayo kwa sasa inapatikana katika jukwaa la filamu la Netflix, ina majibu ya maswali yako, unakosaje?

Na hiyo ndiyo zawadi yako ya christmas kutoka kwa santa wako, Nukta the Podcast.

Kwa niaba ya timu nzima ya Nukta the podcast na  Nukta Afrika kwa ujumla tunakutakia heri ya Krismasi na baraka tele kwa mpya 2022.

Enable Notifications OK No thanks