Fanya haya kabla hujapanga safari ya mapumziko ya mwisho wa mwaka 2022

December 23, 2022 2:14 pm · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Kabla haujapanga safari zingatia gharama za safari,usalama wa eneo unalotembelea pamoja na hali ya hewa
  • Usisahau bima ya afya na fedha ya akiba unapopanga safari zako.

Dar es Salaam. Baada ya kufanya kazi kwa miezi 12, watu wengi huwaza namna wanavyoweza kuipumzisha miili na akili zao huku wakijiandaa na majukumu yanayowasubiri kwa  mwaka mwingine unaofuata wa 2023.

Kuna aina nyingi za kupumzika, wengine hujifungia ndani wakisikiliza muziki waupendao, wengine hupendelea mitoko ya kuangalia filamu huku wengine hupenda kusafiri au kwa kimombo wanasema vacation.

Achana na aina nyingine za kupumzika hapa tunazungumzia aina hii ya safari au vacation ambayo mara nyingi hufanyika mwisho wa mwaka wakati ofisi nyingi zipo mapumziko.

Kwa mujibu wa tovuti ya Allina Health, safari husaidia kuboresha afya ya akili, huongeza furaha, pamoja na kuboresha mahusiano na familia au ndugu ambao mtasafiri pamoja.

Kutokana na faida hizo ni kweli kuwa unahitaji safari, lakini je unafahamu mambo ya kuzingatia kabla hujaamua kwenda sehemu uipendayo kijipumzisha?

Timu ya Nukta Habari (www.nukta.co.tz) imekuandalia mambo ya muhimu ya kuzingatia kabla ya kusafiri kwa ajili ya mapumziko ya mwisho wa mwaka. Twende pamoja!

50,049 Group On Mountain Top Stock Photos, Pictures & Royalty-Free Images -  iStock  Baada yakufanya kazi kwa mwaka mzima ni vyema kupata muda wa kupumzika na kutembelea maeneo mbalimbali. Picha | iStock. 

Gharama za safari

Kabla ya kuanza safari ni vyema kuzingatia gharama za safari husika, ikiwemo nauli ya kwenda na kurudi, gharama za chakula na malazi.

Kwa  wanaopenda kutembelea vivutio vya utalii, ikiwemo mbuga za wanyama zilizopo ndani ya nchi suala la kujua  gharama za kutembelea vivutio hivyo ni la muhimu kwani kuna baadhi ya vivutio utahitaji kutoboa  mfuko zaidi kuvitembelea.

Hata hivyo, kuna meneo mengi unayoweza kuyatembelea kwa gharama ndogo tu na bado ukafurahia mapumziko yako ya mwisho wa mwaka.

Maeneo  hayo ni pamoja na ufukweni, maeneo ya makumbusho, maeneo ya utamaduni na vivutio vingine vinavyoweza kufikiwa kwa urahisi bila kuhusisha gharama kubwa.


Zingatia usalama wa eneo unalotembelea

Wakati unapanga safari ni vyema kuzingatia usalama wa eneo unaloenda kutembelea ili kuhakikisha usalama wako na mali zako wakati wote uwapo safarini.

Moja kati ya vitu vya  kuzingatia ni historia ya usalama wa eneo hilo, ikiwa eneo hilo limeshawahi kuingizwa kwenye rekodi  ya maeneo hatarishi, chukua tahadhari. 

Harlod Mndewa, muongoza watalii katika hifadhi ya Mlima Kilimanjaro anasema kuna baadhi  ya maeneo hayafai kabisa kutembelea licha ya kuwa na mandhari mazuri na vivutio  vingi vya utalii.


Soma zaidi


Namna ya kufika kwenye eneo husika

Kila eneo safari utakayoipanga lazima uzingatie namna ya kufika katika meneo hayo.

Kuna baadhi ya sehemu hazifikiki kwa usafiri wa gari, wala baiskeli hivyo kama haupo vizuri kwenye kutembea kwa miguu unaweza kushindwa kuendelea na safari hiyo.

Kuna safari nyingine zitahitaji usafiri wa ndege, nyingne meli au boti hivyo kusababisha kuongezeka kwa gharama za safari yako. Ikiwa hukujipanga mapema unaweza kuishiwa fedha ukiwa nusu ya safari.

Tovuti ya Global Goode imeanisha mbinu mbalimbali unazoweza kuzitumia kujua jinsi unavyoweza kufika sehemu unazotamani kutembelea ikiwemo kusoma vitabu vya mwongozo (tour guide books).

Mbinu nyingine ni pamoja na kuuliza watu waliowahi kutembelea maeneo hayo, kutazama video na picha za maeneo hayo zilizowekwa mtandaoni na kuuliza watoa huduma wa hoteli uliyofikia ikiwa uzoefu wao kuhusu eneo husika.

Mbali na hayo kuna mbinu nyingine ya kutumia mtandao na teknolojia kujua umbali na sehemu husika unayotaka kutembelea ikiwemo ramani ya Google inayoweza kukupa maelekezo ya sehemu yoyote unayoenda ilimradi tu iwe inatambulika na mtandao huo.

“Mimi  huwa naangalia mtandaoni ili kujua nawezaje kufika sehemu ninayotaka kwenda, hata kama ni kutembea natumia Gooogle map (ramani ya Google) kujua ni dakika ngapi nitatembea,” anasema Pendo Kajuka mtumiaji wa mtandao huo.

man looking at map photo – Free Map Image on Unsplash Kufahamu eneo unaloenda kabla ya kuanza safari kunasaidia kufanya maandalizi ya mapema yanaoendana na eneo unaloenda. Picha | Unsplash.

Zingatia hali ya hewa ya mahali unapotembelea

Kuna baadhi ya maeneo yana hali ya baridi sana au joto. Kushindwa kuzingatia kipengele hiki kunaweza kuharibu safari yako nzima.

Ukiwa umepanga kwenda safari nje ya nchi maeneo yenye baridi au mikoa yenye baridi ikiwemo Nyanda za Juu Kusini, Kanda ya Ziwa na Kaskazini mwa Tanzania  ni lazima kubeba mavazi ya kukinga baridi ili uweze kufurahia safari yako kwenye maeneo hayo.

Ikiwa unatembelea maeneo yenye joto na jua kal,  nguo nzito zitavuruga safari yako.

Kuhakikisha utekelezwaji wa hatua hii, muongoza watalii Harlod Mndewa anasema soma habari za utabiri wa hali ya hewa za maeneo husika au waulize watu wa karibu waliowahi kutembelea maeneo hayo

“Ni bora uulize hata waongoza watalii kuhusu vitu vya kubeba ikiwemo mavazi ili kuzuia usumbufu kutumia fedha zaidi kununua dawa na mavazi yanayoendana na hali ya hewa,” anasema Mndewa ambaye amepanda Mlima Kilimanjaro mara 300

Mbali na mbinu hizo unaweza pia kutumia mtandao kupata taarifa za hali ya hewa za siku husika, wiki au miezi ijayo za  mji wowote unaotamani kwenda.


Tangazo


Hakikisha una bima ya afya

Unapoamua kusafiri maeneo ya mbali na nyumbani lolote linaweza kutokea, unaweza ukaumwa gafla na ikiwa umebeba kadi ya bima ya afya basi unaweza kujihakikishia usalama.

Bima ya afya ikupa urahisi wa kupata hudduma za afya eneo lolote utakaloamua kutembelea kipindi hiki cha mwisho wa mwaka.

Hata hivyo kuna baadhi ya meneo hawatoi huduma za afya kwa kutumia bima hivyo utalazimika kubeba pesa za ziada ili kuweza kupata huduma hiyo.

Enable Notifications OK No thanks