Fahamu: Meya wa London hakupewa chanjo ya Corona

December 24, 2020 8:37 am · TULINAGWE ALSON
Share
Tweet
Copy Link
  • Baadhi ya watu wamemzushia kuwa amepata chanjo ya Corona.
  • Wametumia picha alipoenda kupata chanjo ya mafua Septemba 28, 2020.
  • Watu watakiwa kupata taarifa sahihi kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO).

Dar es Salaam. Kama umekua makini kufuatilia habari mbalimbali zinazotolewa juu ya ugonjwa wa Corona, huenda umeshakutana na video ikionyesha Meya wa Uingereza Sadiq Khan akipewa chanjo inayosemekana ni ya Corona.

Habari hiyo iliyopo kwenye mfumo wa video, inasimuliwa kwa lugha ya Kiswahili kutoka mtandao wa Youtube na chaneli ya Tan Africa Tz inayohusika na kutoa habari mbalimbali inaonyesha kuwa Meya huyo anapata chanjo huku sindano ikiwa na ufuniko wake na kusemekana anapewa chanjo ya Corona.

Hata hivyo, habari hiyo haina ukweli wowote kwa sababu, mpaka hakuna taarifa rasmi ya Serikali ya Uingereza inayoeleza kuwa Khan amepata chanjo ya virusi hivyo vinavyosambaa kwa kasi duniani. 

Video hiyo ya dakika 1 na sekunde 24 inayosambaa mtandaoni imebeba kichwa kinachosema “Pichani ni Sadiq Khan alipokua anafanya maigizo ya kupewa chanjo inayosemekana ni ya Corona virus”,

Hata hivyo, Nukta Fakti kwa kutumi zana za kidijitali imebaini kuwa picha iliyotumika katika habari hiyo ilikuwa ya tukio la Septemba 28, 2020 ambapo Khan alikuwa akipata chanjo ya mafua.

Baada ya kupata chanjo hiyo, meya huyo aliandika ujumbe kwenye ukurasa wake wa Twitter ukisema, “If you or someone you know is entitled to receive a flu jab, remember you can get one for free at your local high street pharmacy or GP surgery” 

Ujumbe huo unamaanisha kuwa “Kila mtu ana haki ya kupata chanjo ya mafua, kumbuka inapatikana bure katika maduka ya dawa karibu yako.”

Pamoja na kwamba matukio hayo ni tofauti lakini picha iliyotumika ni moja. Huo ni uzushi kwa sababu Serikali ya Uingereza haijatoa taarifa rasmi kuhusu Khan kupata chanjo ya Corona.


Zinazohusiana:


Tayari nchi hiyo imeanza kutumia chanjo yake ya Pfizer/BioNTech. 

Habari hiyo, haina ukweli wowote na inalenga kuwapotosha watu kuhusu chanjo ya Corona.

Enable Notifications OK No thanks