Corona: Zingatia haya unapopokea mgeni nyumbani
March 10, 2021 12:41 pm ·
Rodgers Raphael
- Ni pamoja na kuendeleza tabia za kujikinga na corona hata mnapokuwa nyumbani ikiwemo kuvaa barakoa na kunawa mikono.
Dar es Salaam. Miaka mitatu iliyopita, kupokea mgeni nyumbani huenda lilikua jambo la kheri na wageni walipokelewa kwa makumbato mazito kutoka kwa wenyeji wakifurahia ujio wao huku watoto wakishangilia kwa mapokezi tofauti tofauti na kupokea mizigo ya mgeni.
Hata hivyo, huenda tamaduni hizo zikabadilika katika kipindi hiki cha mpito cha ugonjwa wa Corona ambapo kila mtu anatakiwa kuchukua tahadhari kwa kuepuka na mgusano kati ya mtu na mtu ama kitu na mtu bila kuwepo ulazima.
Hata hivyo, maisha ni lazima yaendelee ikiwa ni pamoja na kupokea wageni hasa pale panapokuwa na ulazima wa ugeni huo. Zipo tahadhari ambazo unaweza kuzichukua unapopokea mgeni. Siyo unyanyapaa, ni tahadhari.
Tazama video hii kujifunza zaidi:
Latest

2 days ago
·
Esau Ng'umbi
CCM yaahidi kutengeneza ajira milioni 8 ifikapo 2030

3 days ago
·
Kelvin Makwinya
Bajeti ya Wizara ya Ardhi yapungua kwa Sh7.2 bilioni 2025/26

6 days ago
·
Fatuma Hussein
Bajeti Wizara ya Maendeleo yaongezeka kwa asilimia 11.9

6 days ago
·
Kelvin Makwinya
Tanzania kujenga kituo cha upandikizaji figo kikubwa zaidi Afrika