Wanafunzi kubadilishana ubunifu maonyesho ya teknolojia Dar

August 28, 2018 4:33 pm · TULINAGWE ALSON
Share
Tweet
Copy Link
  • Wanafunzi kutoka Pwani na Dar watakutana ili kubadilishana uzoefu katika sekta ya teknolojia.
  • Yatasaidia kukuza vipaji na ubunifu wa wanafunzi wa shule za sekondari na vyuo vikuu.

Dar es Salaam. Wanafunzi wa shule za sekondari na vyuo Jijini Dar es Salaam wanatarajia kunufaika na elimu ya ubunifu wa miradi ya maendeleo, baada ya Chuo kikuu cha Mtakatifu Joseph kuandaa maonyesho ya siku tatu yatakayowakutanisha wanafunzi hao kubadilishana uzoefu katika sekta mbalimbali ikiwemo sayansi na teknolojia.    

Maonyesho hayo yatafanyika katika viwanja vya Mlimani City kuanzia Agosti 29 hadi 31 mwaka huu ambapo wanafunzi waliofanikiwa kubuni miradi mbalimbali wataonyesha  kazi zao ili kutoa hamasa kwa wanafunzi wanaoendelea na masomo kubuni njia mbadala kutatua changamoto zilizopo kwenye jamii.

Afisa Udahili wa chuo hicho, Johanitha Patrick amesema wanakusudia maonyesho ya mwaka huu yataleta matokeo chanya kwa jamii kwa sababu  wanafunzi watapata fursa ya kubadilishana uzoefu na kujifunza mambo mbalimbali kutoka kwa wataalamu kulingana na malengo waliyonayo katika jamii.

 “Mwitikio ni mkubwa kwasababu wanafunzi wanapata kujifunza kutoka kwa wenzao na miradi iko ya aina mablimbali inayowasaidia wanafunzi kujifunza kwa kubadilishana mawazo,” amesema Joanitha.

Wanafunzi wanaotarajia kushiriki maonyesho hayo ni kutoka mkoa wa Pwani na Dar es Salaam ambapo yatalenga zaidi katika sekta za sayansi na teknolojia ambapo baadhi ya wanafunzi wamegundua njia bora za teknolojia kutatua changamoto za kijamii ikiwemo magari yanayotumia umemejua na gesi kuzima moto.  

Hiyo siyo mara ya kwanza Chuo hicho kuandaa maonyesho hayo imekuwa ikifanya hivyo miaka mitatu iliyopita ikiwa ni muendelezo wa maonyesho ya kila mwaka ya vyuo vya elimu ya juu ambayo huratibiwa na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) na vyuo mbalimbali nchini.

 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa suti) akimsikiliza Mwanafunzi wa mwaka wanne fani ya uhandisi Chuo Kikuu cha Mtakatifu Joseph cha jijini Dar es Salaam, Tumaini Lutufyo (kushoto) wakati alipokuwa anatoa maelezo ya gari la kuzima moto ambalo linatumia gesi lililotengenezwa na wanafunzi wa chuo hicho katika maonyesho ya mwaka 2017. Picha|Fullshangwe.

 

Follow Us on TikTok

Subscribe to Our YouTube Channel

Subscribe

Loading videos...

Loading videos...

Loading videos...

Enable Notifications OK No thanks