Vodacom, Google wazindua manunuzi ya ‘Apps’ kwa njia ya simu

September 13, 2018 8:52 am · Zahara
Share
Tweet
Copy Link
  • Mteja ataweza kununua programu (Apps) kwa kutumia salio lake la simu na hatalazimika kwenda benki tena.
  • Ni njia ya rahisi zaidi ya teknolojia kwa watumiaji wa simu za ‘Android’ kufanya manunuzi mbalimbali wakiwa popote.
  • Inasaidia kuimarisha mfumo wa fedha jumuishi na kuondokana na mfumo wa zamani kubeba fedha mfukoni.

Dar es Salaam. Sasa wapenzi wa programu za simu (Apps) katika duka la Google hawatapata tabu tena ya kufanya malipo baada ya mfumo mpya wa manunuzi kubuniwa na kampuni kubwa za mawasiliano duniani.

Mfumo huo ni ule wa kufanya manunuzi ya Apps kwa njia ya  simu za mkononi bila kulazimika kutumia malipo ya benki ambayo yana mchakato mrefu kidogo.

Hiyoni kutokana na mtandao wa simu wa Vodacom kuingia makubaliano na kampuni ya Google ambayo inamiliki duka la mtandaoni la ‘Play Store’ ambapo wateja wenye vifaa au simu za ‘Android‘ ambao walikuwa wanatumia huduma za kibenki katika kununua programu mbalimbali za simu, sasa wataweza kununua kupitia simu zao moja kwa moja.

Tunafurahi kushirikiana na Google kuleta njia hii rahisi, nyepesi na ya kuaminika ya malipo kwenye  Google Play Store,” amesema Mkuu wakitengoVodacom Tanzania chaMawasiliano na Uhusiano wa Umma, Jacquiline Materu.


Zinazohusiana:  


Hivyo basi wateja wa Vodacom watakuwa na uwanja mpana wakununua maudhui katika Google Play store zikiwemoprogramuzamichezo, muziki, filamu, maonyesho ya runinga (TV)na vitabu vya kielektroniki kwa urahisi zaidi, kwa kutumia salio la simu kwenye mtandao wa Vodacomambapo awali ni kadi za benki tu ndizo zilikuwa zikitumika kufanya manunuzi hayo.

Materu amefafanua kuwa, uvumbuzi huu utarahisisha mchakato wa malipo na kuboresha huduma kwa wateja wake, “kama jukwaa la kuwasilisha maudhui, tunabeba jukumu la kutaarifu, kuelimisha na kuburudisha wateja wetu kwa kutumia tekinolojia. 

Mkuu wa Mawasiliano na Mahusiano ya umma wa Vodacom, Jacquiline Materu (kati) akiwaonesha waandishi wa habari jinsi ya kufanya manunuzi  kwa kutumia salio la simu wakati wa uzinduzi wa ubia huo kati ya Vodacom na Google Play Store jijini Dar es Salaam leo. Wengine ni  Meneja wa Ushirikiano wa Jukwaa la Android Afrika kutoka Google, Cassandra Mensah-Abrampah (kulia) na Mtendaji wa huduma za thamani wa Vodacom, Prestin Lyatonga (kushoto). Picha| Vodacom

Kwa upande wake, Mwakilishi kutoka jukwaa la Google Afrika, Cassandra Mensah-Abrampah amesema wamefurahi kuongeza wigo wa ushirikiano wa malipo ya moja kwa moja baina ya kampuni hizo mbili. 

“Tumefurahi sana kuongeza wigo wa ushirikiano wa malipo ya moja kwa moja baina ya  Google Play Direct na Vodacom Group ikiwa ni pamoja na kufanya uzinduzi huu na Vodacom Tanzania. 

Utozaji kwa njia ya simu ni mojawapo ya nguzo muhimu kwenye ujumuishi wa kifedha katika uchumi wa app ama programu katika masoko kwa sababu  watu wengi bado hawana akaunti za benki,” amesema  Mensah-Abrampah.

Hatua hiyo iliyopigwa na Vodacom ni miongoni mwa mikakati ya kuboresha na kuimarisha mfumo jumuishi  wa kifedha ambao unaziunganisha taasisi za fedha na watoa huduma mbalimbali duniani na kuondokana mfumo wa zamani wa kubeba fedha mfukoni au kwenda benki moja kwa moja. 

Enable Notifications OK No thanks