Rasmi Kamishna Diwani Athumani bosi Takukuru

September 6, 2018 11:03 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Kabla ya uteuzi huo mpya alikuwa Katibu Tawala Mkoa wa Kagera.
  • Pia amewahi kuwa Kamanda wa Polisi katika mikoa ya Shinyanga na Mbeya.
  • Anachukua nafasi ya Kamishna Valentino Mlowola aliyeteuliwa kuwa Balozi.

Kamishna wa Polisi Diwani Athumani rasmi ni Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru). Picha| Mwananchi.

Dar es Salaam. Rais John Magufuli amemteua Kamishna wa Polisi Diwani Athumani kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na utezi wake unaanza rasmi leo Septemba 6, 2018. 

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu, Kamishna Athumani anachukua nafasi ya Kamishna wa Polisi, Valentino Mlowola ambaye ameteuliwa kuwa Balozi. 

Kamishna Athumani aliyewahi kuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), kabla ya uteuzi huo mpya alikuwa Katibu Tawala Mkoa wa Kagera. Pia aliwahi kuwa Kamanda wa Polisi katika mikoa ya Shinyanga na Mbeya.

Kwa upande wake, Kamishna Mlowola chati yake imezidi kupanda ikizingatiwa kuwa aliteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Disemba 2015 baada ya Rais Magufuli kutengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa taasisi hiyo wa wakati huo, Dk Edward Hoseah kutokana na kutoridhishwa na namna taasisi hiyo ilivyokuwa ikitekeleza wajibu wake katika kukabiliana na rushwa hususani kwenye upotevu wa mapato ya serikali katika bandari ya Dar es salaam.  

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
21 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
21 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwanzo mwisho mapokezi ya Rais wa Namibia Netumbo Nandi Ikulu Dar es Salaam

Mwanzo mwisho mapokezi ya Rais wa Namibia Netumbo Nandi Ikulu Dar es Salaam

Nukta TV

Sikia kisa cha bibi wa Mbagala, chanzo Jaji Mkuu Masaju kupanda cheo

Sikia kisa cha bibi wa Mbagala, chanzo Jaji Mkuu Masaju kupanda cheo

Nukta TV

FAHAMU KUHUSU SIKOSELI | Part 1: Ugonjwa wa kurithi, unaotesa maelfu ya watoto Tanzania

FAHAMU KUHUSU SIKOSELI | Part 1: Ugonjwa wa kurithi, unaotesa maelfu ya watoto Tanzania

Nukta TV