Rais Samia kuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya uhuru Msumbiji, Komoro 

June 11, 2025 6:34 pm · Fatuma Hussein
Share
Tweet
Copy Link
  • Ziara hiyo ni sehemu ya juhudi za kuimarisha ushirikiano wa kihistoria na kidiplomasia kati ya Tanzania na mataifa jirani.

Dar es Salaam. Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kufanya ziara katika nchi za Msumbiji na Visiwa vya Komoro ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuimarisha ushirikiano wa kihistoria, kidiplomasia na kiuchumi kati ya Tanzania na mataifa hayo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Juni 11, 2025 jijini Dodoma na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, Rais Samia amepokea mialiko rasmi kutoka kwa Marais wa nchi hizo ili awe mgeni katika maadhimisho muhimu ya kitaifa, yakiwemo ya miaka 50 ya uhuru wa Msumbiji.

“Ziara hizi zinatokana na jitihada kubwa za Mheshimiwa Rais katika kuimarisha uhusiano kati ya Tanzania na mataifa mbalimbali duniani. Msumbiji ni jirani yetu wa kihistoria na ndugu wa damu, hivyo mwaliko huu ni heshima kubwa kwa taifa letu,” amesema Msigwa.

Ziara ya Rais Samia nchini Msumbiji inakuja siku chache tu baada ya Rais wa nchi hiyo, Daniel Francisco Chapo kufanya ziara ya kwanza rasmi Tanzania tangu achaguliwe kushika wadhifa huo Januari 15, 2025. 

Katika ziara hiyo, viongozi hao walishuhudia utiaji saini wa mikataba miwili na hati nne za makubaliano katika maeneo mbalimbali ya ushirikiano ikiwemo biashara, elimu, utamaduni na huduma za kijamii.

Aidha, Rais Samia pia amepokea mwaliko kutoka kwa Rais wa Komoro Azali Assoumani kushiriki maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru wa Muungano wa visiwa hivyo yatakayofanyika Julai 6 mwaka huu.

“Tanzania na Komoro, kama ilivyo kwa Msumbiji ni mataifa ya ndugu yaliyounganishwa na historia ya ukombozi wa Afrika na udugu wa muda mrefu. Ziara hii inalenga kudumisha mshikamano na kukuza fursa za kiuchumi, kiutamaduni na kijamii kwa manufaa ya wananchi wetu,” ameeleza Msigwa.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwenendo wa deni la serikali

Mwenendo wa deni la serikali

Nukta TV

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Nukta TV

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Nukta TV