Rais Samia azindua tume kutathimini migogoro wa ardhi, uhamaji wa hiari Ngorongoro

February 20, 2025 6:28 pm · Fatuma Hussein
Share
Tweet
Copy Link
  • Tume hizo zitaongozwa na Jaji Dk Gerald Ndika pamoja na Mhandisi Musa Iyombe.

Dar es Salaam. Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, amezindua Tume ya Rais ya kutathmini masuala ya mgogoro wa ardhi katika eneo la Hifadhi ya Ngorongoro na tume ya Rais ya kutathmini zoezi la uhamaji wa hiari wa wakazi wa Eneo hilo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Februari 20, 2025 na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu,uzinduzi wa Tume hizo ni utekelezaji wa ahadi aliyoitoa Rais Samia Disemba 1, 2024 alipokukutana na kuzungumza na viongozi na wawakilishi wa wananchi wanaoshi eneo la Ngorongoro na maeneo jirani mkoani Arusha 

Tume ya kutathmini masuala ya mgogoro wa ardhi katika eneo la Hifadhi ya Ngorongoro itaongozwa na Jaji Dk Gerald Ndika, huku tume ya kutathmini zoezi la uhamaji wa hiari wa wakazi wa eneo hilo ikiongozwa na Mhandisi Musa Iyombe.

Sanjari na hilo tume hizo pia zinajumuisha uwakilishi wa wananchi wa eneo la Ngorongoro na zinatarajiwa kukamilisha kazi zao ndani ya kipindi cha miezi mitatu. 

Huenda kuanzishwa kwa tume hizo, kutachochea utatuzi wa mgogoro wa ardhi kati ya Serikali na wananchi wa Ngorongoro ambao umekuwa ukiendelea kwa zaidi ya miaka ishirini bila kupatiwa suluhu kutokana na ukinzani uliopo kati ya mahitaji ya ardhi na sera za Serikali zinazotaka kulinda ikolojia ya eneo hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Enable Notifications OK No thanks