Rais Magufuli akutana na wanasiasa wa upinzani, Mfanyabiashara Rostam Aziz

November 13, 2018 10:01 pm · Zahara
Share
Tweet
Copy Link
  • Rostam aipongeza Serikali uboreshaji wa miundombinu ikiwemo reli, barabara na bandari ambayo ni muhimu katika kuzalisha ajira na ukuaji wa uchumi.
  • Wapinzani wamsifia Rais Magufuli kwa ujasiri na misimamo katika maamuzi ikiwemo utatuzi wa bei ya korosho.
  • Wamuahidi kuendelea kumpa ushirikiano katika kutimiza ajenda za maendeleo.

Dar es Salaam. Rais John Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na mfanyabiashara Rostam Aziz pamoja na baadhi ya wanasiasa wa upinzani ili kujadili mambo mbalimbali yanayohusu hali ya kisiasa na mwenendo wa shughuli za uchumi nchini.

Wanasiasa hao ambao wamekutana na Rais Magufuli leo (Novemba 13, 2018) Ikulu Jijini Dar es Salaam ni pamoja na Mwenyekiti wa chama cha NCCR-Mageuzi na Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia nchini (TCD) James Mbatia; Mwenyekiti wa Baraza la vyama vya siasa, John Shibuda; na Mwenyekiti wa chama cha United Democratic Party (UDP), John Cheyo.

Baada ya mazungumzo hayo Rostam amempongeza Rais Magufuli kwa uongozi bora na uboreshaji wa miundombinu ikiwemo reli, barabara na bandari ambayo ni muhimu katika kuzalisha ajira na ukuaji wa uchumi.

“Tunamuunga mkono Rais kwa kuhakikisha watanzania tunawekeza katika nchi yetu, kukuza uchumi wetu, hilo ndilo la msingi kwa sisi wafanyabiashara,” amesema Rostam.

           

Kwa upande wake, Mbatia  amesema kuwa Tanzania inafanya vizuri katika malengo 17 ya maendeleo endelevu, huku akibainisha lengo la elimu bora na shirikishi lipewa kipaumbele na akaeleza umuhimu wa kuwepo kwa umoja na upendo nchini.

“Watanzania wote wana kila sababu ya kuendelea kuijenga nchi yao kwa mawazo ya pamoja ya ujumbe  uliopo katika wimbo wa Taifa, unaosisitiza amani, umoja na upendo,” amesisitiza Mbatia.


Zinazohusiana:


Vilevile Shibuda amempongeza Rais Magufuli kwa hatua alizozichukua katika utatuzi wa soko la korosho na kumhakikishia kuwa vyama vya siasa vinamuunga mkono katika kurekebisha dosari na mmomonyoko wa maadili ndani ya serikali na vyama vya siasa.

“Rais Magufuli amerejesha sifa ya utaifa wetu ya kuwa nchi ya kuaminika na kusadikika na amekweza hali ya uhuru na kujitegemea,” amesema Shibuda.

Naye Cheyo hakuacha kumpongeza Rais Magufuli kwa kuwa na moyo wa ujasiri katika kuchukua maamuzi magumu katika  miaka mitatu ya uongozi wake tangu alipoingia madarakani mwaka 2015.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
21 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
21 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
21 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwanzo mwisho mapokezi ya Rais wa Namibia Netumbo Nandi Ikulu Dar es Salaam

Mwanzo mwisho mapokezi ya Rais wa Namibia Netumbo Nandi Ikulu Dar es Salaam

Nukta TV

Sikia kisa cha bibi wa Mbagala, chanzo Jaji Mkuu Masaju kupanda cheo

Sikia kisa cha bibi wa Mbagala, chanzo Jaji Mkuu Masaju kupanda cheo

Nukta TV

FAHAMU KUHUSU SIKOSELI | Part 1: Ugonjwa wa kurithi, unaotesa maelfu ya watoto Tanzania

FAHAMU KUHUSU SIKOSELI | Part 1: Ugonjwa wa kurithi, unaotesa maelfu ya watoto Tanzania

Nukta TV