“Queen and Slim”: Filamu mahususi kwa sikukuu ya wapendanao

February 14, 2020 6:55 am · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link

kukutana kwa mara ya kwanza yaani “first date” ya Slim (Daniel Kaluuya) na mpenzi wake mpya Queen (Jodie Turner-Smith) yanaishia katika mauji. Picha| BBC.


  • Ni filamu inayozungumzia juu ya penzi jipya kati ya mwanadada Queen na kijana Slim.
  • Safari ya mapenzi yao inaanza vibaya baada ya Slim kumuua askari polisi kwa risasi.

Dar es Salaam. Ule msemo wa “mimi na wewe dhidi ya dunia” au “You and me against the world” ndiyo unashika hatamu katika filamu hii ya “Queen and Slim”.

Huenda ukayaita mapenzi yenye bahati mbaya kwani kukutana kwa mara ya kwanza yaani “first date” ya Slim (Daniel Kaluuya) na mpenzi wake mpya Queen (Jodie Turner-Smith) kunaishia katika mauji.

Usiogope! Aliyeuawa siyo Queen wala Slim. Ni askari polisi ambaye aliwasimamisha kwa sababu ya makosa ya barabarani. 

Baada ya Slim kumuua polisi huyo kwa bastola, taarifa za wawili hao zinasambaa kwenye mitandao ya kijamii huku watu wakiwabatiza jina la wauwaji wa polisi.

Wapenzi hao wanapita vihunzi na kuuvuka mlima huo wa majaribu kwa pamoja huku penzi lao jipya likizidi kupamba moto.

Maandamano yanayotaja majina yao, vikosi vya askari polisi vinavyowatafuta, mapenzi yanayochochewa mithiri ya moto wa vifuu vya nazi kwenye upepo. Hivyo ni baadhi ya vitu utakavyovifurahia katika filamu hii mahususi kwa wapendanao.


Zinazohusiana


Unaachaje kujinyima Sh10,000 kutazama filamu iliyoongozwa na mwanadada Melina Matsoukas mwenye tuzo zaidi ya 20 huku video za muziki alizosimamia zikiwa ni video zilizopamba chati za muziki duniani.

Ndiyo! Ninaongelea video za muziki zikiwemo “Im Into You” yake Jenifer Lopez pamoja na “Formation” na “Pretty Hurts” zake Beyonce,

Hakika kuitazama na mpenzi wako filamu hii inayokadiriwa kugharimu takriban Sh46.2 bilioni ni kitu kizuri kufanya hasa kama unataka kuimarisha mahusiano yako na yule umpendaye hata katika mapito mnayopitia hasa kipindi hiki cha sikukuu ya wapendanao.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
13 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
13 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
13 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: HII HAPA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027

🔴LIVE: HII HAPA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027

Nukta TV

Mashine za kukaushia rangi za kucha kutozwa ushuru kwa asilimia 10

Mashine za kukaushia rangi za kucha kutozwa ushuru kwa asilimia 10

Nukta TV

Wazee wa 'kubet' hii inawahusu, 5% kutozwa kwenye dau la kamari

Wazee wa 'kubet' hii inawahusu, 5% kutozwa kwenye dau la kamari

Nukta TV