Petroli, mafuta ya taa vyachangia kushusha mfumuko wa bei

September 9, 2019 2:00 pm · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Kasi ya mfumuko wa bei za bidhaa na huduma umeshuka hadi kufikia asilimia 3.6 kwa mwaka ulioishia Agosti 2019 kutoka asilimia 3.7 iliyorekodiwa Julai mwaka huu.
  • Kushuka huko kumechangia zaidi na kupungua kwa gharama za bidhaa zisizo za chakula ikiwemo petroli na mafuta ya taa.

Dar es Salaam. Kasi ya mfumuko wa bei za bidhaa na huduma nchini Tanzania umeshuka hadi kufikia asilimia 3.6 kwa mwaka ulioishia Agosti 2019 kutoka asilimia 3.7 iliyorekodiwa Julai mwaka huu, ikichagizwa zaidi na kupungua kwa gharama za bidhaa zisizo za chakula.

Mfumuko wa bei wa Taifa hupima kiwango cha kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi nchini.

Ripoti ya mfumuko wa bei ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) iliyotolewa leo (Sepetemba 9, 2019), imeeleza kuwa kushuka kwa mfumuko wa bei kumechangiwa na kupungua kwa mfumuko wa bei za bidhaa hasa zisizokuwa za chakula ikilinganishwa na Julai mwaka huu.

Mfumko wa bei  wa bidhaa zisizo za chakula ambazo umeshuka ni pamoja na mafuta ya taa ambayo yamepungua kwa asilimia 2.6, petroli kwa asilimia 4.3 na majiko ya gesi kwa asilimia 1.4,

Pia gharama za kufanya ukarabati wa nyumba (1.7) na bidhaa za usafi binafsi ikiwemo mafuta ya nywele (1.3).


Zinazohusiana: Mfumuko wa bei wang’ang’ania kiwango cha Januari


Kwa upande wa bidhaa za vyakula na vinywaji, mfumuko wa bei umeongezeka hadi asilimia 3.7 kutoka asilimia 2.9 kama ilivyorekodiwa Julai 2019.

Sambamba na bidhaa hizo, bidhaa na huduma zingine kama hoteli, migahawa na huduma za elimu hazijabadilika kabisa huku huduma za tamaduni na mapumziko (recreation) zikishuka kwa asilimia 0.4.

“Kushuka kwa mfumuko wa bei kunaelezea kuwa kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka zimeishia ulioishia mwezi Agosti 2019.”  inasomeka sehemu ya ripoti ya mfumuko wa bei ya NBS iliyotolewa Jumatatu (Septemba 9, 2019)

NBS imesema kasi ya mabadiliko ya bei ya Agosti 2019 ipo chini ikilinganishwa ni ile iliyorekodiwa Julai 2019.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
13 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
13 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
13 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: HII HAPA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027

🔴LIVE: HII HAPA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027

Nukta TV

Mashine za kukaushia rangi za kucha kutozwa ushuru kwa asilimia 10

Mashine za kukaushia rangi za kucha kutozwa ushuru kwa asilimia 10

Nukta TV

Wazee wa 'kubet' hii inawahusu, 5% kutozwa kwenye dau la kamari

Wazee wa 'kubet' hii inawahusu, 5% kutozwa kwenye dau la kamari

Nukta TV