Panga pangua ya Rais Samia kwa wakuu wa wilaya hii hapa

January 25, 2023 10:44 am · admin
Share
Tweet
Copy Link
  • Wakuu wa wilaya wapyaa 37 wateuliwa, 48 wahamishwa vituo vya kazi huku 55 wakisalia kwenye vituo vyao
  • Hamdu Shaka, Jafar Haniu na Dina Mathamani ni miongoni mwa walioteuliwa. 

Dar es Salaam. Huenda leo ikawa ni siku ya shangwe, nderemo na huzuni kwa baadhi ya watu, mara baada ya Rais wa Tanzania kufanya mabadiliko ya Wakuu wa wilaya nchini ikiwemo kuteua wapya na kuwafuta kazi 37.

Mmoja wa watu waliochomoza katika mkeka wa Rais Samia ni aliyekuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Shaka Hamdu Shaka ambaye ametuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kilosa.

Shaka aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kilosa amechukua nafasi ya Majid Hemed Mwanga aliyepelekwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mlele mkoani Katavi. 

Shaka aliondolewa katika wadhifa huo baada ya  kuhudumu kwa muda wa mwaka mmoja na miezi tisa akichukua nafasi ya Humphrey Polepole ambaye kwa sasa ni Balozi wa Tanzania nchini Malawi.

Nafasi ya Shaka amechukuliwa na Sophia Mjema. 

Mabadiliko hayo yamehusisha uteuzi wa wakuu wa wilaya wapya 37, kuwahamisha vituo vya kazi wakuu wa wilaya 48 huku 55 wakisalia kwenye vituo vyao vya kazi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu leo Januari 25, 2022, kati ya wakuu wa wilaya hao 140, wanawake ni 40 au sawa na asilimia 28.5.


Soma zaidi:


Wakuu wa Wilaya wapya

Wengine wapya 36 walioteuliwa ni Felician Gasper Mtahengerwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha na Marko Henry Ngu’mbi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Longido,

Emmanuela Kaganda Mtatifikolo ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha huku Gerald Mongella akipelekwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Chemba mkoani Dodoma.

Katika orodha hiyo ya wakuu wa wilaya wapya, Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Zuhura Yunus amesema Kanali Boniphace Magembe ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Geita, Leah Lucas Ulaya kawa Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe, Deusdedith Josephat Katwale anakuwa Mkuu wa Wilaya Chato.

Mwandishi wa Habari wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Grace Henry Kingalame anaenda Wilaya ya Nyang’halwe huku Dk Linda Peniel Salekwa  akiteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa. 

Wengine ni Dk Abel Mwendawile Nyamahanga  aliyeteuliwa  kuwa Mkuu wa Wilaya ya Muleba, Japhet Mosses Maganga anaenda Wilaya ya Kyerwa,  Erasto Yohana Sima kuwa Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Julius Kalanga Laiser – kuwa Mkuu wa Wilaya ya Karagwe, huku Dinah Elias Mathamani  akiteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Uvinza.

Dk Christopher David Timbuka  naye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Siha mkoani wakati mwenzake Amir Mohamed Mkalipa anaenda kuongoza Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro. 

Kasilda Jeremia Mgeni sasa ni Mkuu wa Wilaya ya Same, Goodluck Asaph Mlinga kuwa Mkuu wa Wilaya ya Liwale huku Chistopher  Ngubiagai kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kilwa na Beno Morris Malisa ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbeya mkoani Mbeya.

Katika mkeka huo wa wakuu wa wilaya wapaya yupo pia Josephine Keenja Manase ambaye anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Kyela na aliyewahi kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu Jaffar Mohamed Haniu sasa ni Mkuu wa Wilaya ya Rungwe.

Rebeca Sanga Msemwa  ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Morogoro na Rachel Stephen Kasanda ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Magu mkoani Mwanza.

Aliyekuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Shaka Hamdu Shaka ambaye ametuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kilosa. Picha | CCM Blog.

Hassan Omary Bomboko  naye  ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe, Victoria Charles Mwanziva  ameenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ludewa huku Kanali Joseph Samwel Kolombo akiteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kibiti na Zephania Stephan Sumaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mafia mkoani Pwani.

Lazaro Killian Komba ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kalambo, Dk Jane Chacha Nyamsenda ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga,  Wilman Kapenjama Ndile kuwa Mkuu wa Wilaya ya Songea, Mboni Mohamed Mhita kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kahama na  Farida Salum Mgomi  ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ileje.

Orodha hiyo ndefu imetamatika kwa Solomon Jonas Itunda ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Songwe, Zakaria Saili Mwansasu  kuwa Mkuu wa Wilaya ya Uyui na wa mwisho ni Naitapwaki Lumeya Tukai  ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Nzega mkoani Tabora.

Itakumbukwa Septemba 30, mwaka 2022, Rais Samia aliwataka wakuu wa wilaya nchini kutimiza majukumu yao ipasavyo baada ya kupata taarifa kuwa baadhi yao hawafanyi kazi ila wanasubiri orodha mpya ya wakuu wa wilaya.

“Napata meseji huku hawafanyi kazi wapo kama wamepigwa ganzi. Nilisema tulichofanya ni uchambuzi wa utendaji wenu tumjue nani mzuri nani mbaya, aliyesema anataka kuwabadilisha nani?,” alisema Rais Samia.

Tangu mwaka 2023 uanze Rais Samia amekuwa akifanya mabadiliko katika sehemu mbalimbali ikiwemo ikulu na katika taasisi nyeti za ulinzi na usalama nchini ikiwemo aliyofanya jana ya kumfuta kazi Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Reuben Ndiza Mfune na wakurugenzi wa halmashauri nne.

Waliohamishwa vituo

Miongoni mwa waliohamishwa vituo ni Thomas Cornel Apson aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Siha amepelekwa Ikungi kuchukua nafasi ya Jery Muro ambaye ametenguliwa. 

Suleiman Yusufu Mwenda  amehamishwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Monduli Kutoka Wilaya ya Iramba. Edward Jonas Mpogolo amekuwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala akitokea Same pamoja na Halima Abdallah Bulembo aliyehamishwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni kutoka Muheza mkoani Tanga.

Hashim Abdallah Komba  amepelekwa kuingoza Wilaya ya Ubungo akitokea  Nachingwea, Mwanahamisi Athumani Mukunda amekuwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke kutoka Wilaya ya Bahi huku Saadi Ahmed Mtambule anaenda Kinondoni kutoka  Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa. 

Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Sophia Mfaume Kizigo amehamishwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa, huku Godwin Crydon Gondwe akihamishwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Bahi kutoka Wilaya ya Kinondoni na  Veronica Arbogast Kessy amehamishwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Iringa ikitokea Misungwi.

ACP Advera John Bulimba  amepelekwa Biharamulo akitokea Nzega, Majid Hemed Mwanga amekuwa Mkuu wa Wilaya ya Mlele kutoka Wilaya ya Kilosa.

Salum Hamis Kalli amekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kigoma kutoka Wilaya ya Magu na Kisare Matiku Makor sasa atakuwa Mkuu wa Wilaya ya Moshi akitokea Wilaya ya Uyui.

Mohamed Hassan Moyo  aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Iringa sasa amehamishwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, huku Kherry Denis James akipelekwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbulu akitokea Ubungo jijini Dar es salaam.

Rais Samia pia amewahamisha Dk Vicent Naano Anney kuwa Mkuu wa Wilaya ya Bunda kutoka wilayani Rungwe, Kanali Denis Filangali Mwila ameenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbarali akitokea Ukerewe ambapo sasa anachukua nafasi ya Reuben Ndiza ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Sebastian Muungano Waryuba sasa atakuwa  Mkuu wa Wilaya ya Malinyi akitoka Wilaya ya Sumbawanga. Danstan Dominic Kyobya amehamishwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kilombero kutoka Wilaya ya Mtwara na Dk Julius Keneth Ningu  sasa atakuwa Mkuu wa Wilaya ya Ulanga akitokea Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma.

Orodha hiyo pia imemtaja aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Liwale, Judith Martin Nguli amepelekwa Mvomero huku Hanafi Hassan Msabaha akihamishwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mtwara kutokea Wilaya ya Uvinza.

Lauter John Kanoni sasa ni Mkuu wa Wilaya ya Masasi akitokea Wilaya ya Wanging’ombe mkoani Njombe ambapo nafasi yake imechukuliwa na Claudia Undalusyege Kitta.

Hivi sasa Matiko Paul Chacha atakuwa Mkuu wa Wilaya ya Misungwi akitokea Kaliua mkoani Tabora.  Ng’wilabuzu Ndatwa Ludigija atakuwa Mkuu wa Wilaya ya Kwimba akitokea Wilaya ya Ilala huku Fatma Almas Nyangasa akihamishwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe na kuchukua nafasi ya Nick Simon John ambaye amehamishiwa Kibaha.

Halima Habib Okash amehamishwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo kutoka Wilaya ya Mvomero, Filberto Hassan Sanga amehamishwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Nyasa akitokea wilayani Mlele na Ngollo Ng’waniduhu Malenya amehamishwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo akitokea Ulanga.

Johari Musa Samizi aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kwimba sasa atakuwa Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Simon Peter Simalenga atakuwa Mkuu wa Wilaya ya Bariadi akitokea Wilaya ya Songwe na Anna Jerome Gidarya atakuwa Mkuu wa Wilaya ya Busega akitokea  Wilaya ya Ileje.

Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke Jokate Mwegelo sasa amehamishwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, na Moses Joseph Machali atakuwa Mkuu wa Wilaya ya Mkalama akitokea Bukoba.

Kemilembe Rose Lwota sasa atakuwa Mkuu wa Wilaya ya Manyoni, Singida  akitokea Wilaya ya Biharamulo, Joshua Samwel Nassari kuwa Mkuu wa Wilaya ya Iramba akitokea Bunda , pamoja na Esther Alexander Mahawe  kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbozi akitokea  Wilaya ya Kigoma.

Orodha ya waliohamishwa imetamatishwa na Dk Mohamed Rashid Chuachua aliyehamishwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kaliua, Said Mohamed Mtanda aliyehamishwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Urambo huku Louis Peter Bura kuwa Mkuu wa Wilaya ya Tabora. 

Wengine ni Albert Gasper Msando aliyehamishwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Handeni akitokea Wilaya ya Morogoro huku Zainab Abdallah Issa akihamishwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Pangani akitokea wilayani Bagamoyo.

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Rais Samia azindua minara 758, aacha maagizo mazito juu ya mkongo wa taifa

Rais Samia azindua minara 758, aacha maagizo mazito juu ya mkongo wa taifa

Nukta TV

JAJI MKUU: Njia za asili ni mojawapo ya njia halali za utatuzi wa migogoro

JAJI MKUU: Njia za asili ni mojawapo ya njia halali za utatuzi wa migogoro

Nukta TV

Hesabu ya bosi, bei ya mafuta pasua kichwa madereva wa daladala

Hesabu ya bosi, bei ya mafuta pasua kichwa madereva wa daladala

Nukta TV