NEMC yatoa siku 90 kwa watoa huduma za afya kuboresha miundombinu ya taka hatarishi

May 16, 2024 10:35 am · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Yasema itafanya ukaguzi katika vituo vyote nchini kubaini utekelezaji wa agizo hilo.
  • Watakaokaidi kuchukuliwa hatua ikiwemo kufungiwa vituo vyao.

Dar es Salaam. Baraza la Taifa la Kuhifadhi wa Mazingira (NEMC) limetoa siku 90 kwa watoa huduma za afya kuboresha miundombinu ya kuhifadhi taka hatarishi ili kulinda wananchi na madhara yatokanayo na kuzagaa kwa taka hizo.

Kwa mujibu wa NEMC Taka hatarishi ni zile zinazopatikana baada au wakati utoaji wa huduma za afya ikiwemo nyembe, sindan, mipira ya maji na damu, madawa yaliyotumika, baadhi ya viungo, migando ya damu na nyingine zinazofanana na hizo.

Mkurugenzi wa Uzingatiaji na Utekelezaji wa Sheria NEMC, Hamad Kissiwa aliyekuwa akizungumza na waandishi wa habari leo Mei 16, 2024 jijini Dar es Salaam amesema endapo watoa huduma hao hawatazingatia kanuni za utunzaji mazingira wanaweza kusababisha madhara kwa wananchi.

“Tumekuta pia taka hizo zinatupwa porini na baadhi zinachomwa kwa moto wa wazi matokeo yake zinaleta hatari kwenye maisha ya binadamu na wanyama, madhara makubwa yanayoweza kutokana na hii kulipa hasara taifa letu,” amesema Kissiwa.

Wakati NEMC ikitoa angalizo hilo, katika jamii kumeshuhudiwa kukithiri kwa utupaji hovyo wa taka hizo hatarishi katika maeneo ya umma ikiwemo fukwe jambo linaloweza kusababisha mlipuko wa magonjwa na aina nyingine za magonjwa zinazohusisha muingiliano wa bakteria au vijidudu.


Soma zaidi:Ripoti: Afya ya akili chanzo cha watu kujiua, kuua Tanzania


Watakaokaidi kukiona

Kissiwa amesema baada ya kipindi hicho walichokitoa kwa ajili ya maboresho kuisha NEMC litafanya ziara katika vituo vyote vya afya nchini na watakaokaidi watachukuliwa hatua.

“Wale wote watakao kiuka adhabu itatolewa ikiwemo hata kusimamishwa huduma zake ili waweze kufanya marekebisho kuokoa mazingira yetu afya zetu pamoja na kulinda rasilimali za nchi yetu,” amesema Kissiwa. 

Aidha, NEMC imewataka wato huduma za afya kuacha kuwatumia watoa taka wasio thibitishwa badala yake kutumia wakandarasi walioidhinishwa na Wizara ya Afya kwa kuwa wana maeneo mahususi kwa ajili ya shughuli hiyo.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwenendo wa deni la serikali

Mwenendo wa deni la serikali

Nukta TV

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Nukta TV

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Nukta TV