Nchimbi Katibu Mkuu mpya CCM

January 15, 2024 4:07 pm · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Nchimbi anarithi nafasi ya Daniel Chongolo aliyejiuzuru Novemba 27, 2023.
  • Akuwa katibu mkuu wa 12 tangu CCM ianzishwe.

Dar es Salaam. Chama Cha  Mapinduzi (CCM)  kimemteua Emmanuel Nchimbi kuwa Katibu Mkuu mpya wa chama hicho akiziba pengo la Daniel Chongolo aliyejiuzulu Novemba 27  mwaka Jana.

Uteuzi huo umefanyika leo Januari 15, 2024 katika kikao cha Halmashauri Kuu ya chama hicho ikiyokutana Zanzibar kwa ajili ya kujadili ajenda mbalimbali za chama hicho na kumteua Nchimbi ambaye ndiye mtendaji mkuu wa shughuli zote za chama.

Uteuzi huo wa Nchimbi umekuja ikiwa imepita miezi minne tangu amalize muda wake katika nafasi ya Balozi wa Tanzania nchini Misri, nafasi aliyoitumikia kwa mwaka mmoja tangu Machi, 2022.

Nchimbi aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM anakuwa Katibu Mkuu wa 12 kukitumikia chama hicho tangu ilipoanzishwa mwaka 1977 na wa pili tangu Rais Samia Suluhu aingie madarakani Machi, 2021.

Viongozi wengine walioshika nyadhifa hiyo ni pamoja na Pius Msekwa kuanzia mwaka 1977-1981, Daudi Mwakawago (1981-1982), Rashid Kawawa (1982-1990) na Horace Kolimba kuanzia mwaka 1990 hadi 1995.

Wengine ni Laurence Gama kuanzia mwaka 1995-1997, Philip Mangula (1997-2007), Yusuf Makamba (2007-2011), Wilson Mukama (2011-2012), Abdulrahman Kinana (2012-2018), Bashiru Ally (2018-2021)
Na wa mwishoni Daniel Chongolo kuanzia mwaka 2021 hadi Novemba 2023.

Mambo yanayomsubiri Nchimbi
Nchimbi anaingia madarakani wakati ambapo CCM inakabiliana na masuala nyeti ikiwemo uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Madiwani unaofanyika mwaka huu pamoja na Uchaguzi Mkuu wa maraisi na wabunge mwakani.

/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
5 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
5 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Unaweza kusema ni maumivu juu ya maumivu kwa watumiaji wa vyombo vya moto vinavyotumia mafuta ya

Unaweza kusema ni maumivu juu ya maumivu kwa watumiaji wa vyombo vya moto vinavyotumia mafuta ya

Nukta TV

Neema Mohamed, Mkurugenzi wa Bone and Blood Foundation, ni shujaa wa ugonjwa wa selimundu Sickl

Neema Mohamed, Mkurugenzi wa Bone and Blood Foundation, ni shujaa wa ugonjwa wa selimundu Sickl

Nukta TV

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, ametua kwenye ardhi ya Urusi kwa ziara ya kitaifa ya siku

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, ametua kwenye ardhi ya Urusi kwa ziara ya kitaifa ya siku

Nukta TV