Mhadhiri UDSM ateuliwa kuwa mwenyekiti bodi ya NBS

September 25, 2019 11:16 am · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Rais John Magufuli amemteua Dk Amina Msengwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) akichukua nafasi ya mtangulizi wake, Adrew Masawe.
  •  Dk Msengwa alikuwa Mhadhiri na Mkuu wa Idara ya Takwimu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Dar es Salaam. Rais John Magufuli amemteua Dk Amina Msengwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) akichukua nafasi ya mtangulizi wake, Adrew Masawe.

Kwa mujibu wa taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu iliyotolewa leo (Septemba 25, 2019), uteuzi huo umefanyika baada ya Masawe kumaliza muda wake katika kuitumikia bodi hiyo.

Kabla ya uteuzi huo, Dk Msengwa alikuwa Mhadhiri na Mkuu wa Idara ya Takwimu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). 

Follow Us on TikTok

FOLLOW NOW

Subscribe to Our YouTube Channel

SUBSCRIBE NOW