Mfumuko wa bei wapaa na kuvunja rekodi

August 10, 2022 5:15 am · Daniel Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Umefikia asilimia 4.5 kwa mwaka ulioshia Julai 2022.
  • Kiwango hicho Trading Economics inasema ni cha chini zaidi kuwahi kurekodiwa Tanzania tangu Oktoba 2017.
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa imesema bidhaa za vyakula zimechangia kwa kiasi kikubwa kupanda kwa kasi ya bei ya bidhaa na huduma.

Dar es Salaam. Kasi ya mfumuko wa bei za bidhaa na huduma nchini imepanda hadi kufikia asilimia 4.5 kwa mwaka ulioishia Julai 2022 kutoka asilimia 4.4 iliyorekodiwa Juni mwaka huu, ikichagizwa zaidi na kupanda kwa bei ya baadhi ya bidhaa za vyakula.

Kiwango hicho cha Julai kilichotangazwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) jana Agosti 9, 2022 ni cha kihistoria kwa kuwa ni cha juui zaidi kuwahi kurekodiwa nchini tangu Oktoba 2017 kwa mujibu wa tovuti ya Trading Economics. Oktoba 2017 mfumuko ulikuwa asilimia 5.1.

Mfumuko wa bei wa Taifa hupima kiwango cha kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi nchini.

“Kuongezeka kwa mfumuko wa bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia mwezi Julai, 2022 kumechangiwa hasa na kuongezeka kwa mfumuko wa bei wa baadhi ya bidhaa za vyakula kwa kipindi cha mwaka ulioishia mwezi Julai, 2022 ikilinganishwa na kipindi cha mwaka ulioishia mwezi Juni, 2022,” imeeleza NBS katika taarifa yake.

Baadhi ya bidhaa za vyakula zilizoonesha kuongezeka kwa mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi Julai, 2022 ikilinganishwa na mwaka ulioishia mwezi Juni, 2022 ni pamoja na mchele kutoka asilimia 14  hadi asilimia 16.8, mahindi (kutoka asilimia 30.9 hadi asilimia 44.6) na  unga wa mtama kutoka asilimia 4.4 hadi asilimia 4.7.

Mfumuko wa bei ya unga wa mahindi umeongezeka kutoka asilimia 12.9 hadi asilimia 19.3, nyama ya kuku (kutoka asilimia 4.7 hadi asilimia 5.7), dagaa wakavu (kutoka asilimia 4.6 hadi asilimia 5.7), karanga (kutoka asilimia 12.2 hadi asilimia 14.1) na unga wa muhogo kutoka asilimia 5.6 hadi asilimia 9.5.

Baadhi ya bidhaa zisizo za vyakula zimeonesha kupungua kwa kasi ya mfumuko wa bei katika kipindi cha mwaka ulioishia mwezi Julai, 2022 ukilinganishwa na mwaka ulioishia mwezi Juni, 2022 ni pamoja na dizeli kutoka asilimia 49.6 hadi asilimia 42.1, petroli (kutoka asimilia 32.8 hadi asilimia 29.2), mafuta ya taa (kutoka asilimia 52.7 hadi asilimia 48.4) na gesi ya kupikia kutoka asilimia 13.8 hadi asilimia 9.4. 

“Mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mwaka ulioishia mwezi Julai, 2022 umeongezeka hadi asilimia 6.5 kutoka asilimia 5.9 kwa mwaka ulioishia mwezi Juni, 2022,” imeeleza NBS. 

Mfumuko wa Bei ambao haujumuishi bidhaa za Vyakula na Vinywaji baridi kwa mwezi Julai, 2022 umepungua kidogo hadi asilimia 3.8 kutoka asilimia 3.9 ilivyokuwa mwezi Juni, 2022.


Zinazohusiana: 


Afrika Mashariki hali ikoje?

Nchini Uganda, mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi Julai, 2022 umeongezeka hadi asilimia 7.9 kutoka asilimia 6.8 kwa mwaka ulioishia mwezi Juni, 2022 huku Kenya, mfumuko wa bei umeongezeka hadi asilimia 8.3 kutoka asilimia 7.9.  

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: RAIS SAMIA ANAZINDUA MELI YA KWANZA YA UVUVI WA BAHARI KUU

🔴LIVE: RAIS SAMIA ANAZINDUA MELI YA KWANZA YA UVUVI WA BAHARI KUU

Nukta TV

Kwa nini wanawake wako katika hatari zaidi kupata magonjwa ya akili?

Kwa nini wanawake wako katika hatari zaidi kupata magonjwa ya akili?

Nukta TV

🔴LIVE: HOMERA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA BUNGENI

🔴LIVE: HOMERA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA BUNGENI

Nukta TV

BENEFIT FROM
Nukta ADS
Advertise with us to reach a wider audience with high conversion rates.
Other Nukta Africa Products
Nukta Habari
Stories that matter
Topics
Inuldge yourself with the topics in Nukta
All
Business
Africa
Contact
Tel
+255 750 881 888
Mail
newsroom@nukta.co.tz
Address
Mwananyamala kwa Kopa Dabe House Dar es Salaam TZ, 14108
Social Media

© 2024 Nukta Africa. All Rights Reserved.