Mauzo ya parachichi nje ya nchi yapaa kwa 236%

October 9, 2026 5:19 pm · Method Allen
Share
Tweet
Copy Link
  • Hiyo ni sawa na kusema mauzo ya parachichi nje ya nchi yameongezeka zaidi ya mara mbili  ndani ya kipindi cha takribani miaka sita.

Dar es Salaam. Msimu wa zao la parachichi kwa mwaka 2025/2026 umeanza kwa kicheko kwa wakulima, baada ya mauzo ya zao hilo kupaa kwa asilimia 236.9 ndani ya kipindi cha miaka sita, suala linalotoa muelekeo chanya wa sekta hiyo nchini.

Waziri wa Kilimo Daniel Chongolo, aliyekuwa akifungua mkutano wa tatu wa kitaifa wa wadau wa tasnia ya parachichi uliofanyika Dodoma amesema uzalishaji uliofanyika katika msimu wa 2025/2026 umevuka lengo la mwaka.

“Tanzania iliuza nje tani 52,000 za parachichi, kiasi kilichovuka lengo la tani 40,000 lililowekwa na kutarajiwa kufikiwa ifikapo mwaka 2030,” amesema Chongolo Oktoba 7, 2026.

Mwaka 2020/2021, Tanzania iliuza nje tani 15,432.77 za parachichi, kabla ya kiasi hicho kuongezeka hadi tani 52,000 mwaka 2025/2026.

Kwa mujibu wa Chongolo mauzo ya tani 52,000 mwaka 2025/2026 yameingiza Dola za Marekani milioni 97.2 sawa na Sh259.5 bilioni ulikinganisha Dola za Marekani milioni 44.2 ambayo ni sawa na Sh118 bilioni kwa viwango vya sasa katika msimu wa mwaka 2020/2021. | Picha Daily News

Hiyo ni sawa na kusema mauzo ya parachichi nje ya nchi yameongezeka zaidi ya mara mbili  ndani ya kipindi cha takribani miaka sita, hali inayoashiria kuimarika kwa nafasi ya Tanzania katika soko la kimataifa la zao hilo.

Parachichi yapaisha fedha za kigeni

Kwa mujibu wa Chongolo mauzo ya tani 52,000 mwaka 2025/2026 yameingiza Dola za Marekani milioni 97.2 sawa na Sh259.5 bilioni ulikinganisha Dola za Marekani milioni 44.2 ambayo ni sawa na Sh118 bilioni kwa viwango vya sasa katika msimu wa mwaka 2020/2021.

Kwa mujibu wa takwimu hizo, mapato hayo yameongezeka kwa asilimia 120.4 ndani ya kipindi cha miaka sita.

Hii inaonyesha kuwa ukuaji wa tasnia ya parachichi hauishii katika kuongeza kiwango cha zao linalofika masoko ya nje, bali pia unaongeza mchango wake katika upatikanaji wa fedha za kigeni nchini.

Sababu zatajwa

Akizungumzia sababu za ukuaji huo, Waziri Chongolo amesema mafanikio hayo yamechangiwa kwa kiasi kikubwa na ushirikiano kati ya Serikali na sekta binafsi katika kuimarisha tasnia ya parachichi.

Alisema hatua hizo zimehusisha kuboresha miundombinu, kuimarisha mifumo ya masoko na kuweka mifumo rasmi, yenye uwazi na ufanisi katika mnyororo mzima wa thamani wa zao hilo.

Hata hivyo, kuvuka lengo la tani 40,000 lililowekwa kwa mwaka 2030 kunaiweka Tanzania katika hatua nyingine ya safari yake ya kutoka kuongeza kiasi cha parachichi kinachozalishwa hadi kuhakikisha wakulima na wadau wengine wananufaika zaidi na soko hilo linalokua.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
5 Oct, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
5 Oct, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
BoT: Vita Mashariki ya Kati vyaathiri bei ya mafuta na mbolea, soko la dunia

BoT: Vita Mashariki ya Kati vyaathiri bei ya mafuta na mbolea, soko la dunia

Nukta TV

BoT yashikilia CBR 6.25% kudhibiti mfumuko wa bei

BoT yashikilia CBR 6.25% kudhibiti mfumuko wa bei

Nukta TV

Bei ya mafuta yapaa, petroli yafikia Sh4,057

Bei ya mafuta yapaa, petroli yafikia Sh4,057

Nukta TV