Mauzo ya bidhaa, huduma za Tanzania nje ya nchi yapaa

September 12, 2019 12:08 pm · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Ongezeko la mauzo ya bidhaa na huduma nje ya nchi limechochewa na bidhaa zisizo za asili kwa asilimia 80 ya bidhaa zote zilizouzwa nje ya nchi
  • Dhahabu peke yake imechangia asilimia 40 ya bidhaa ambazo sio za asili baada ya ongezeko la mauzo yake nje ya nchi kuongezeka kwa asilimia 23.3.

Dar es Salaam. Mauzo ya bidhaa na huduma za Tanzania nje ya nchi yameongezeka hadi kufikia zaidi ya Sh19.7 trilioni katika mwaka unaoishia Julai 2019 kutoka Sh19.6 trilioni iliyorekodiwa Julai mwaka uliopita, yakichagizwa zaidi na bidhaa zisizo za asili. 

Ripoti ya Mapitio ya Uchumi ya mwezi Agosti 2019 (Monthly Economic Review) iliyotolewa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT), ongezeko la mauzo ya bidhaa na huduma zimechangiwa zaidi na bidhaa zisizo za asili ambazo mauzo yake yalikuwa asilimia 80 ya bidhaa zote zilizouzwa nje ya nchi.

Bidhaa zisizo za asili ni pamoja na madini ya dhahabu na bidhaa za viwandani. 

Bidhaa hizo ambazo zisizo za asili zimeongezeka kutoka Sh 7.1 trilioni kwa mwaka wa Julai 2018 hadi kufikia Sh8.5 trilioni Julai mwaka huu.

Dhahabu peke yake imechangia asilimia 40 ya bidhaa hizo baada ya mauzo yake kuongezeka kwa  asilimia 23.3 katika kipindi cha mwaka mmoja.


Zinazohusiana


Wakati mauzo ya bidhaa zisizokuwa za asili yakiongezeka, mauzo ya bidhaa za asili yameporomoka kutoka Sh2.5 trilioni Julai 2018 hadi Sh1.1 trilioni kwa mwaka unaoishia Julai 2019. 

Ripoti hiyo imeainisha kuwa bidhaa zote za asili zimeathirika kimauzo isipokuwa kahawa na pamba. 

Kwa mujibu wa BOT, ipo mipango ya kukabiliana na hali hiyo ikiwemo kuongeza kiasi cha kuuza bidhaa nje ya nchi. 

Kwa upande wa manunuzi ya bidhaa na huduma nje ya nchi, ripoti hiyo imeonyesha kuwepo kwa ongezeko la kuingiza bidhaa na huduma za nje ya nchi ambapo ongezeko hilo limefikia Sh24.1 trilioni kwa mwaka unaoishia Julai 2019 kutoka Sh22.7 trilioni.

Bidhaa zinazoingizwa nchini ni pamoja na bidhaa zinazotumika katika ujenzi wa miundombinu ikiwemo reli na madaraja, bidhaa za mafuta ambazo zinachukua asilimia 23.1.

/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
5 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
5 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Wabunge waliokwenda Morocco bila kibali kikaangoni , utoro ukiibuliwa bungeni

Wabunge waliokwenda Morocco bila kibali kikaangoni , utoro ukiibuliwa bungeni

Nukta TV

Mfahamu Leonard Mususa Alama ya Ungozi iliyoacha majonzi kwa 'MACEOs' Tanzania

Mfahamu Leonard Mususa Alama ya Ungozi iliyoacha majonzi kwa 'MACEOs' Tanzania

Nukta TV

Bei za mafuta mwezi Juni hizi hapa, dizeli ikipaa kwa Sh85

Bei za mafuta mwezi Juni hizi hapa, dizeli ikipaa kwa Sh85

Nukta TV